WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema hatua ya kuhusishwa
kwake na Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania)
ni upuuzi na mwendelezo wa mikakati ya kumchafua.
Kauli ya Lowassa imekuja siku moja baada ya kuhusishwa na Mbunge wa
Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), kwamba kwa pamoja wamekuwa
wakipanga mikakati ya siri ya kuhujumu chama hicho.
↧