Wakili wa Serikali, Yasinta Rwechungula (44) Mkazi wa Boko njia panda, anayekabiliwa na kesi ya kumpiga na kumjeruhi mfanyakazi wake wa ndani ameendelea kusota rumande kutokana na kutotimiza masharti ya dhamana.
Hakimu wa Mahakama ya Mkazi Kinondoni, Amaria Mushi, alimtaka kuwa na wadhamini wawili kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh milioni nne.
↧