Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Arusha (RCC) kimetaka polisi na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, kuacha kutoa matamko ya haraka, badala yake wachunguze kubaini chanzo cha milipuko ya mabomu jijini Arusha.
Miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema aliyesema matukio hayo si ya siasa, bali yanayodhuru jamii, hivyo ni vyema polisi wanapopewa
↧