FAMILIA mbili mjini Mpanda zimejikuta zikiingia katika uhasama mkubwa, kiasi cha kupigana fimbo na ngumi makaburini katika ugomvi wa kugombea kuzika mwili wa mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.
Sababu kubwa ya mpasuko huo imeelezwa kuwa ni mahari, kwani wazazi wa upande wa mama wa mtoto huyo walikuja juu na kumzuia baba wa mtoto, Joseph Bacho mkazi wa Mtaa wa Kawajense- Madukani
↧