Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ameonja chungu
ya uamuzi wa Serikali wa kusitisha mikutano ya hadhara katika mikoa ya
Lindi na Mtwara baada ya kushindwa kufungua mashina ya chama hicho mjini
Mtwara.
Nape ambaye alikuwa mkoani Mtwara kwa ziara ya
siku moja, alijikuta akiishia kuwakabidhi bendera za chama hicho
viongozi wa matawi ili wakazipandishe wenyewe kimyakimya.
↧
Mikutano ya Nape Nnauye yapigwa Marufuku Mtwara.......Alalamika na kusema huko ni kubaka demokrasia
↧