Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, anasubiriwa wiki hii kutegua kitendawili cha hoja za wabunge, kuhusu punguzo la kodi katika mishahara, vyanzo vipya vya mapato na utekelezaji wa miradi wa maendeleo.
Leo ndio siku ya mwisho kwa wabunge kujadili hotuba ya bajeti ya Waziri Saada na kesho Waziri ataanza kujibu hoja akishirikiana na Naibu wake, Mwigulu Nchemba na Adam Malima.
↧