Rais Jakaya Kikwete amesema mfumo wa vyama vingi vya siasa ni mzuri, umeleta matumaini kwa kupanua wigo na kufungua zaidi uwanja wa kisiasa na kuiwajibisha Serikali.
Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa ili mfumo huo uboreshwe zaidi na uweze kuimarisha misingi mikuu ya maendeleo, ni lazima uendeshwe kwa watu kufuata sheria na wala siyo kuingiza matumizi ya nguvu, ambayo yanaweza
↧