Katika hali inayoashiria ukubwa wa tatizo la ajira katika sekta rasmi nchini, wasomi wa ngazi ya Chuo Kikuu 10,500 walijitokeza jana (pichani) kwenye usaili wa Idara ya Uhamiaji nchini inayohitaji kuajiri watu 70 tu.
Wengi wakiwa ni vijana wasomi wa fani mbalimbali wenye umri wa kati ya miaka 22 na 30, walifurika kwenye uwanja huo uliopo Kurasini, katika Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam
↧