Ofisa wa polisi mwenye cheo cha Koplo, Wilson Mwakipesile wa
Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Kilimanjaro amefariki dunia ghafla
akiwa ndani ya daladala alilokuwa amelikamata.
Hata hivyo, haikujulikana mara moja iwapo trafiki
huyo alifariki dunia akiwa njiani kulipeleka gari hilo kituo cha polisi,
alifariki muda mfupi baada ya kufika kituoni au wakati anapelekwa
hospitali.
↧