Mafuriko yaliyotokea Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki yamesababisha vifo vya watu 41.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema vifo 25 vimethibitishwa. Ameagiza polisi kufanya uchunguzi zaidi kubaini watu wengine ambao hadi sasa hawaonekani waliko.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, eneo la Ilala, vilitokea vifo 11 ingawa inahisiwa watu wengine wawili hawaonekani.
↧