POLISI saba kutoka wilayani Kasulu,
wamepandishwa kizimbani katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, iliyoanza
kikao chake mjini Kigoma leo na kusomewa mashitaka ya kuua kwa
kukusudia.
Mbele ya Jaji Sam Rumanyika, askari Polisi hao walidaiwa kuwa
Agosti 6, 2011 walimpiga na kumuua kwa makusudi Festo Stephano, mkulima
na mkazi wa Kijiji cha Rungwe mpya wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
↧