Wakati Ikulu ikitangaza kwamba Rais Jakaya Kikwete amevunja Tume
ya Mabadiliko ya Katiba, tume hiyo imetoa ufafanuzi wa baadhi ya maeneo
ya Rasimu ya Katiba.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana, ilieleza kuwa
Tume ya Jaji Joseph Warioba ilivunjwa tangu Machi 19, ikiwa ni siku moja
baada ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba bungeni mjini Dodoma.
↧