WATU wanne wameuawa mkoani Mwanza kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe Katika eneo la Igwambiti kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino
Mlowola amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa
11 alfajiri ambapo wananchi walipata taarifa ya kuwepo kwa wizi wa
ng’ombe katika kitongoji cha Mtende.
↧