Madereva wa
daladala Manispaa ya Morogoro wamegoma asubuhi hii wakidai kukamatwa
hovyo na matrafiki na hakuna daladala linalofanya safari yoyote katika
manispaa hiyo.
Madereva
hao wanadai wameamua kugoma kutokana na kamatakamata ya askari wa
usalama barabarani, ambapo wamesema daladala moja kwa siku linaweza
kukamatwa hadi mara nne na wakihoji wanaambiwa ni makosa tofauti.
↧