Victoria Kimani, mrembo na mwanamuziki raia wa Kenya amekana
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na CEO wa Wasafi Classic, Diamond
Platinumz kufuatia tetesi zilizozagaa baada ya wawili hao kuonekana
kwenye picha kadhaa za pamoja.
“Sifahamu hizi tetesi zimetokea wapi. Nilikutana na Diamond mara
moja, na ilikuwa wakati tunarekodi wimbo wa ONE Campaign Afrika Kusini
wiki mbili zilizopita.”
↧