Serikali
imetangaza kuwajiri walimu wapya 36,071 mwaka huu ambao majina yao
yanatarajia kutangazwa katikati ya mwezi huu (Machi) na watatakiwa
kwenda kuripoti katika vituo vyao vya kazi Aprili mosi mwaka huu.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim
Majaliwa, aliyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha
Kumepambazuka jana kinachorushwa na Radio One
↧