Madai ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba
kutaka nyongeza ya posho ya vikao vya Bunge hilo yamegonga mwamba.
Habari kutoka ndani ya kamati iliyoundwa na
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho ili
kufuatilia madai hayo, zimedai kuwa baada ya uchunguzi wa kina, wajumbe
wa kamati hiyo hawakuona sababu ya kupendekeza posho hizo kupandishwa.
↧