Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya tatu kwa ufaulu kitaifa katika
Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne wa 2013, jana alipoteza
fahamu kwa muda baada ya kupata matokeo hayo.
Mwanafunzi huyo, Joyceline Marealle wa Shule ya
Sekondari Canossa ya Dar es Salaam, alipatwa na mkasa huo muda mfupi
baada ya mwandishi wa gazeti hili kumpigia simu na kumweleza matokeo
hayo.
↧