Serikali inatarajia kupeleka kikosi kimoja cha Jeshi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) huko Sudan Kusini kwa ajili ya kulinda amani
kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe alisema Dar es Salaam jana kwamba Serikali
imekubali kupeleka batalioni moja baada ya kuombwa na Umoja wa Mataifa
(UN).
↧