MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CHADEMA, Grace Tendega, amemuwekea pingamizi mgombea mwenzake kupitia CCM, Godfrey Mgimwa, kwa kile kinachodaiwa kuwa si raia wa Tanzania.
Tendega alichukua fomu ya kumwekea pingamizi hilo juzi wakati zoezi la kusitisha fomu za wagombea ukiwa umefikia kikomo. Jana majira ya mchana mgombea huyo alirudisha fomu ya pingamizi kwa msimamizi wa uchaguzi
↧