Rais Jakaya Kikwete jana alitangaza rasmi kuwa Bunge la Katiba litaanza Februari 18, mwaka huu.
Aidha, alisema kuwa atatangaza majina ya wajumbe wa Bunge hilo leo.
Akizungumza kwenye kikao maalumu cha Baraza la Vyama vya Siasa jijini
Dar es Salaam jana, Rais Jakaya Kikwete alisema maandalizi kwa ajili ya
Bunge hilo yanaendelea vizuri na kilichobaki ni marekebisho madogo
madogo.
↧