Askari polisi F. 5264 PC Sabato (37) wa Kituo cha Polisi cha
Longido, wilayani Monduli, ameuawa kwa kupigwa jiwe na mtuhumiwa
aliyekuwa akimpeleka mahabusu katika Gereza la Kisongo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus
Sabas, alisema mauaji hayo yamefanywa na mtuhumiwa aliyekuwa akipelekwa
mahabusu baada ya kukosa dhamana katika kesi ya kuvunja na kuiba.
↧