Chama Cha Mapiduzi (CCM), kimetishia
kuwatimua mara moja, wanachama wasaliti na wasiokubali kushindwa wakati
wa kura za maoni za kuwania kuteuliwa ili kugombea urais, ubunge na
udiwani.
Tishio hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa
chama hicho, Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kata
ya Nsalaga jijini Mbeya.
↧