WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amekiri kwamba Serikali ilifanya uzembe
katika kutatua taarifa za uchochezi zilizosababisha vurugu za Mtwara.
Kauli hiyo aliitoa mjini Mtwara jana alipozungumza na wananchi wa Masasi
akiwa njiani kuelekea wilayani Nanyumbu kufungua mradi wa umeme. Alisema
baada ya kutokea kwa uzembe huo wako wajanja wachache waliotumia nafasi
hiyo kufanikisha malengo yao.
↧