Wakazi sita wa Dar es Salaam maarufu Mbwa Mwitu au waanzilishi
wa kundi la Watoto wa Mbwa, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya
Ilala kujibu shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga aliwataja
washtakiwa hao kuwa ni Sijali Abdallah (19), Sadick Mpambe (25) maarufu
Chitemo na Balozi Inasio (19) wote wakazi wa Kiwalani.
↧