Wafugaji 12 wa jamii ya Kimasai
wilayani Kiteto, katika Mkoa wa Manyara, wamefikishwa mahakamani
wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wakulima tisa.
Mwendesha Mashtaka Sajenti wa Polisi, Oscar
Munisi, alidai kuwa watuhumiwa walitenda makosa hayo Januari 12 mwaka
huu, katika Vitongoji cha Laitime na Mtanzania wilayani Kiteto.
↧