MZAHA unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wilayani Kiteto na
mkoani Manyara katika kusuluhisha mgogoro wa wafugaji na wakulima,
umesababisha mauaji ya watu zaidi ya 13 usiku wa kuamkia jana.
Mbali ya vifo hivyo, vita hiyo iliyaonza majira ya saa 11 alfajiri
kwa kutumia silaha za moto na jadi, imesababisha majeruhi zaidi ya 50
huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu.
↧