POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam imetangaza leo kufanya doria kwa kutumia helikopta ili kuangalia hali ya usalama katika jiji hilo katika sikukuu ya Mwaka Mpya.
Aidha, imepanga kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama, ikiwa ni pamoja na Kikosi cha Zimamoto na uokoaji na vikundi vya ulinzi shirikishi kuhakikisha kunakuwepo udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo
↧