MKUU wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe, amekerwa na tabia ya
watendaji wengi wa serikali kutowajibika ipasavyo na matokeo yake
kuwabebesha mizigo mawaziri na Rais.
Alisema chanzo cha wizara nyingi kutofanya vizuri kunasababishwa na
mfumo mbaya ulioendekezwa na baadhi ya wakurugenzi,makamishna, makatibu
na watendaji walioko chini yao kukosa uzalendo wa kuwajibika kwa
wananchi.
↧