Taharuki na hofu ya moto imewakumba wakazi wa jiji la Dar es Salaam
maeneo ya katikati ya jiji kufuatia Moshi mkubwa uliokuwa ukitoka
katika mojawapo ya majengo ya benki kuu ya Tanzania na kusababisha
baadhi ya wakazi hao pamoja na jeshi la polisi akiwemo kamanda wa jeshi
la polisi mkoa wa kipolisi wa Ilala kufika haraka katika eneo la tukio
kutokana na hofu ya kuungua kwa benki hiyo.
↧