UANACHAMA wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe umetajwa kuwa ‘kaa la moto’ kwa uongozi wa chama hicho hata kabla ya kiongozi huyo kujibu mashitaka 11 yanayomkabili ili kunusuru uanachama wake.
Duru za siasa ndani ya chama hicho, zinasema Chadema haiko tayari kukabiliana na mtikisiko wa Zitto kuvuliwa uanachama, kwa kuwa hatua ya kuvuliwa madaraka tayari imegharimu umoja
↧