HATIMAYE binti anayedaiwa kubakwa na Mbunge wa Urambo Magharibi,
Profesa Juma Kapuya (CCM), amefungua jalada Polisi dhidi ya mbunge huyo.
Habari za kipolisi ambazo Tanzania Dama limezipata, zinasema kuwa binti
huyo ambaye anadai kubakwa na kisha kutishiwa kuuawa na Profesa Kapuya,
amefungua jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi
Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
↧