Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk
Sengondo Mvungi utawasili nchini leo 12.50 jioni kwa ndege ya Shirika la
Ndege Afrika Kusini (Saa) ukitokea Afrika Kusini.
Msemaji wa Tume hiyo, Omega Ngole alisema baada ya
mwili huo kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,
Dar es Salaam utapelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Lugalo.
↧