Watanzania Agness Masogange na Melisa Edward waliokamatwa kwa
kutuhumiwa kubeba dawa za kulevya huko Afrika Kusini wameachiwa kwa
dhamana.
Mkuu wa Kitengo cha Dawa za Kulevya Afrika Kusini,
Kamishna Toto Mangaleni aliithibitishia Mwananchi jana kuwa watuhumiwa
hao wameachiwa kwa dhamana,lakini wataendelea kubaki Afrika Kusini
wakati kesi yao ikiendelea.
↧