Urusi
na Ufaransa zimeeleza wazi wazi tofauti zao kuhusu ripoti ya wataalamu
wa silaha wa Umoja wa Mataifa, ambayo ilithibitisha kwamba silaha za
kemikali zilitumiwa nchini Syria. Waziri wa mambo ya nchi za
nje wa Urusi Sergei Lavrov ambaye alikutana na mwenzake wa Ufaransa
Laurent Fabius mjini Moscow jana, alitupilia mbali madai kwamba serikali
ya Syria ndio iliyotumia silaha hizo
↧