Padri wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Joseph
Monesmo Magamba amemwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa
wa Mlandege jana jioni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi,
Haji Hana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba kiongozi huyo
wa dini amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, akiendelea na matibabu
↧