Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema itafungua mashtaka
dhidi ya kampuni ya Gold Star, baada ya meli yake kukamatwa na tani 30
Za mihadarati aina ya bangi Kisiwa cha Malta Vessel, nchini Italia.
Hatua hiyo ilitangazwa na Mkurugenzi wa Mamalaka
ya Usafiri Baharini (ZMA), Abdi Omar Maalim, alipozungumza ofisini kwake
Mlandege Zanzibar, jana.
↧