Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak Afariki Dunia

$
0
0
Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak ambaye aliitawala Misri kwa takribani miaka 30 kabla ya kuondolewa kwa nguvu, amefariki Dunia Hospitalini, Cairo akiwa na miaka 91.

Televisheni ya taifa imesema Mubarak amekufa hospitali mjini Cairo ambako alikuwa akifanyiwa upasuaji. Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu upasuaji huo.

Hosni Mubarak alikuwa kiongozi wa Misri ambaye kwa karibu miaka 30 alikuwa nembo ya uthabiti katika eneo la Mashariki ya Kati kabla kulazimishwa na jeshi kujiuzulu.

Alilazimishwa kufanya hivyo kufuatia siku 18 za maandamano ya nchi nzima yaliyokuwa sehemu ya vuguvugu la mapinduzi ya msimu wa mapukutiko katika nchi za kiarabu mnamo mwaka 2011.

Televisheni ya taifa imetangaza kuwa Mubarak amefariki akiwa na umri wa miaka 91. 

Muda wote wa utawala wake, alikuwa mshirika wa karibu wa Marekani, akipambana vikali dhidi ya uasi wa makundi ya itikadi kali za kiislamu na mlinzi wa mkataba wa amani kati ya Misri na Israel.

Lakini kwa maelfu na maelfu ya Wamisri vijana walioandamana kwa siku 18 mabarabarani katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo na kwingineko mwaka 2011, Mubarak alikuwa kama farao.

Bondia Deontay Wilder Amtupia Lawama Kocha Wake Baada Ya Kutandikwa na Tyson

$
0
0
Bondia Deontay Wilder amemfukuza kazi kocha wake Mark Breland kufuatia kupigwa TKO round ya 7 vs Tyson Fury na kupoteza Ubingwa wa Dunia uzito wa juu WBC.

Wilder anaamini Mark alikosea kurusha taulo ulingoni kuashiria kuwa Wilder hawezi kuendelea tena na pambano

January Makamba Afunguka...."Watanzania Wanaujua Mchango Wangu na Inatosha"

$
0
0
Mbunge wa Bumbuli na aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba, amesema kuwa idadi kubwa ya Watanzania wanatambua mchango wake katika suala zima la kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki, hata kama viongozi wengine wasipotambua.

Hayo ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, wakati akimjibu mwananchi aliyehoji kauli ya Waziri wa sasa Azzan Zungu, aliyedai kuwa suala la mifuko hiyo lilisimamiwa na viongozi wa juu bila kumtaja Makamba.

“Waziri hayuko wrong ni kweli viongozi wetu hao walitusimamia kwenye suala hili, kuhusu kutambua mchango wangu, karibu Watanzania wote wameutambua na hao kwangu wanatosha, hofu yangu ni kama tutashindwa kusimamia mafanikio yaliyopatikana na mifuko ya plastiki ikarejea mitaani” Makamba.

Hivi karibuni mara baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, Waziri Zungu alisema kuwa licha ya Serikali kupiga marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki, lakini mifuko hiyo imeanza kurejea tena sokoni.

ZOLA kuzawadia vifaa vya umeme wanafunzi wataofanya vizuri katika mitihani yao wilayani Kisarawe

$
0
0

Kampuni ya kuzalisha vifaa vya umeme wa jua ya ZOLA Electric Tanzania, ambayo zamani ilijulikana kama Mpower, imeeleza dhamira yake ya  kusaidia jamii na kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha sekta ya elimu ambapo  imetangaza kuwazawadia vifaa vya nishati ya umeme wa jua wanafunzi wa kidato cha nne watakaofanya vizuri kwenye mtihani wa Taifa katika wilaya ya Kisarawe mwaka huu kupitia kampeni yake inayoendelea inayojulikana kama ‘Bukua na Ushinde’.

Akitangaza ofa hiyo ,Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ZOLA Tanzania, Yusuph Nassoro,amesema  ‘Bukua na Ushinde’Imelenga kuchochea motisha kwa wanafunzi waliopo mashuleni kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu mitihani yao vizuri hususani katika maeneo yenye changamoto ya nishati ya umeme kutoka gridi ya taifa.
 
“Kampuni yetu tunaamini kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na jamii ikielimika, inaweza kupiga hatua ya maendeleo kwa haraka,ndio maana tumekuja na mpango huu wa kutoa motisha kwa wanafunzi mashuleni, hususani maeneo yenye changamoto ya nishati ya umeme ikiwa ni moja ya sera yetu ya kusaidia jamii sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu nchini”,alisema Nassoro.

Alisema wanafunzi watakaofanikiwa kuingia katika 10 bora katika mithani ya taifa ya majaribio watapatiwa zawadi ya vifaa vya kusomea na wanafunzi watatu watakaofanikiwa kuingia katika  3 bora watafungiwa mitambo ya umeme wa sola kwenye familia zao sambamba na kupatiwa vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati hiyo kutoka kampuni ya ZOLA.

Nasoro,alisema mpango huo wa kusaidia wanafunzi utafanyika katika wilaya mbalimbali nchini ambako kampuni hiyo inaendesha shughuli zake, katika siku za  karibuni ilitangaza ofa hiyo kwa wanafunzi wa sekondari katika wilaya ya Longido, mkoani Arusha.
 
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, ameipongeza kampuni ya Zola, kwa kubuni mpango huu wenye lengo la kuinua sekta ya elimu kupitia kutoa motisha kwa wanafunzi “Nawapongeza Zola kwa kuja na ubunifu huu ambao utachangia kuinua sekta ya elimu katika maeneo ya vijijini vilevile kwa kuikumbuka wilaya  ya Kisarawe”alisema.
 
 Aliwataka wanafunzi kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili ziwasaidie kupata mafanikio na kukamilisha ndoto zao na watambue kuwa kusoma kwa bidii na kupata maarifa ni moja ya njia itakayowapeleka katika kupata mafanikio katika Maisha yao sambamba na kutoa mchango wa kuendeleza Taifa.
 
Alimalizia kutoa wito kwa makampuni mengine ya biashara kusaidia huduma za kijamii zenye mwelekeo wa kuleta mabadiliko sambamba na kubuni biashara zinazochochea kuongeza fursa za ajira na kujiajiri kama ilivyo kampuni ya Zola.
 
Kampuni ya ZOLA Electric, ambayo zamani ilijulikana kama Mpower ilianza kutoa huduma zake nchini mwaka 2012  ikiwa inatoa huduma za neshati ya umeme wa jua na kuuza vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati hiyo

Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Bunda Ajiunga Na CCM Leo

$
0
0
Diwani kutoka Kata ya Hunyari iliyopo Halmashauri ya Bunda mkoani Mara Makina Josephat ametangaza kuhama Chadema na kuhamia CCM.

Makina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Bunda na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hiko kikuu cha upinzani ametangaza uamuzi wake huo leo jijini Dodoma na kupokelewa na MNEC wa CCM, Ismail Jamaa.

Akizungumza baada ya kumpokea Diwani huyo, MNEC Jamaa amesema wamempokea kiongozi huyo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa na kwamba taratibu zingine za kumpokea zitafanyika wilayani Bunda ambapo anaishi.
 
Nae Makina amesema kwa miaka minne ambayo Rais Dk John Magufuli ameongoza amegusa kila sekta na kumaliza ajenda zote ambazo wapinzani walikua wakizipigania hivyo haoni haja tena ya kuendelea kuwepo upinzani.

Arusha: Ng’ombe Azaa Ndama Mwenye Vichwa Viwili, Midomo Miwili Na Macho Matatu

$
0
0
Na Woinde Shizza, Arusha
TAHARUKI kubwa imeibuka kwa wananchi wa Kijiji cha Ngiresi kilichopo kwenye Kata ya Sokoni 2 katika Halmashauri ya Arusha baada kuzaliwa ng'ombe mwenye vichwa viwili ,midomo miwili na macho matatu .
 
Kuzaliwa kwa ng'ombe huyo katika eneo hilo kumeibua maswali mengi yasiyo na majibu kwa wananchi hao huku wengi wao wakionekana kushangaa.

Akizungumzia tukio hilo, Mmiliki wa ng'ombe huyo Eliakimu Mungasi amesema kwamba wakati anapewa taarifa ya kuzaliwa kwa ng'ombe huyo alipata mshutuko mkubwa kwani haijawahi kutokea katika maisha yake na kwamba ng'ombe huyo amezaliwa Februari 3 mwaka huu na hadi sasa ametimiza siku 23.

Amesema huu ni uzao wa tano wa ng'ombe aliyezaa ndama huyo ambaye amewashangaza wengi na kwamba huko nyuma ng'ombe wote waliozaliwa walikuwa salama na hawana tatizo lolote.

"Watu wanaongea mengi, wengine wanasema ni mambo ya ushirikina kwa maana ya uchawi, wengine wanasema ni laana lakini mimi sijali, nachojua ni mpango wa Mungu na tutaendelea kumtunza,"amesema Mungasi

Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashaur ya Arusha Arusha Charles Ngiroriti amesema hali hiyo ni kawaida kutokea kwa wanyama.Katika utungaji wa kiumbe inaweza ikatokea cell zikagawanyika ,kama vile zilitaka kutengeneza viumbe viwili.

Ameongeza lakini zikishindwa kigawanyika na kufika mwisho ndio anatokea kiumbe wa aina hiyo na kwamba hali hiyo haiuhusiani na imani za kishirikina, hivyo watu waache kuzusha maneno.

Makonda: Zitto Kabwe ni Kibaraka na Ntapambana Naye

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa hana mashaka na kuwa Rais Magufuli ataendelea kushikilia nafasi hiyo, kwani hana mpinzani kutokana na utendaji wake wa kazi.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Februari 25, 2020, wakati akifungua mkutano wa Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC), uliowakutanisha Wabunge, Madiwani, Mameya pamoja na Wakuu wa Wilaya kwa lengo la kujadili na kutokomeza kero mbalimbali ndani ya Mkoa huo.

"Rais atakayeendelea kuongoza Taifa hili anajulikana, kuna siku nikamsikia mtu anajitangaza kule atachukua fomu ya kugombea Urais, nikasema wakimpitisha huyu kwenye chama chao mimi nitamuomba Dkt Magufuli nihangaike naye, huwezi ukamchukua Dkt Magufuli ukamshindanisha na kibaraka anayesimama kwenye jukwaa eti naye anagombea Urais wa nchi" amesema Makonda.

Hivi karibuni Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema kuwa anayo nia ya dhati ya kugombea Urais na kuiongoza nchi, endapo wenzake wataridhia yeye kupeperusha bendera hiyo.

Nafasi za Kazi 92 TANESCO...Mwisho wa Kutuma Maombi ni March 1, 2020

$
0
0

QUALIFICATION AND EXPERIENCE

Form IV and/or VI Secondary School Academic Certificates with Electrical Installation Trade Test Level II and III. Valid Driving License Class C, C1, C2, C3 and/or E will be an added advantage.
_________________________


QUALIFICATION AND EXPERIENCE

• Form IV and/or VI Secondary School Academic Certificates with Basic and/or Professional Driving Certificate from National Institute of Transport (NIT) & and/or VETA;
• Valid Driving License Class C/C1/C2/C3 and/or E;
• Trade Test Grade II or III I in Automobile Engineering/Mechanics from recognized institution is an added advantage;
__________________________


QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Bachelor Degree either in Marketing, Business Administration (majoring in Marketing or Public Relations) or Mass Communication and Public Relations from recognized Institution; Computer knowledge is compulsory; and relevant working experience of one (1) year in a reputable organization.
_____________________


QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Ordinary Diploma in Electrical Engineering from recognized institution. A driving license class C, C1, C2 and E will be an added advantage. 
_____________________ 

==>>Kwa Nafasi Zingine Nyingi Zikiwemo za Mabenk, Makampuni Binafsi <<BOFYA HAPA>>


Watu Wanne Watiwa Mbaroni Kwa Tuhuma Za Wizi Wa Mabilioni Ya Fedha Za Benki Ya NBC

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUKAMATWA WATUHUMIWA WANNE WA WIZI WA MABILIONI YA BENKI YA NBC JIJINI DSM

______________________

Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu wanne waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya G4S Security kwa tuhuma za wizi wa Tsh 1.280,000,000/=,USD402,000 na Euro 27,700. Watuhumiwa hao ni;

1. CHRISTOPHER CLEOPHACE RUGEMALILA (34) dereva wa G4S, mkazi wa Chanika

2. MOHAMEDI ATHUMANI RAMADHANI (40) mlinzi G4S, mkazi wa mtoni kijichi

3. IBRAHIMU RAMADHANI MAUNGA (49), Mlinzi G4S, mkazi wa kiluvya.

4. SALIMU SHAMTE (45) mkazi wa Mbagala kizuiani.

Mnamo tarehe 07/02/2020 watuhumiwa watatu ambao ni

CHRISTOPHER RUGEMALILA, MOHAMEDI ATHUMANI na IBRAHIMU MAUNGA wakiwa na gari namba T 728 BAN, NISSAN HARD BODY, mali ya kampuni ya G4S, Gari la kusindikiza fedha.

Walinzi hao walikabidhiwa fedha kutoka tawi la benki ya NBC Kariakoo na NBC samora ili wazipeleke makao makuu ya benki ya NBC yaliyopo posta ya zamani sokoine drive, lakini hawakufanya hivyo, matokeo yake walipanga njama na kuelekea maeneo ya Temeke Maduka mawili karibu na kituo cha mafuta cha CAMEL na kuchukua fedha zote na kupakia kwenye gari ndogo T.134 DHY Toyota IST ikiendeshwa na SALUMU SHAMTE. Watuhumiwa hao baada ya kufanikisha uhalifu huo walitelekeza gari la Kampuni ya G4S, silaha mbili mali ya G4S, moja aina ya pump action, na bastola moja, mashine ya kuhesabia fedha na muhuri wa Benki ya CBA kisha kuondoka kusikojulikana.

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam baada ya kupata taarifa hizo liliunda kikosi kazi na kuanza ufuatiliaji mara moja, ambapo tarehe 17/02/2020 majira ya mchana huko Mongo la ndege Mtuhumiwa wa kwanza aitwaye CHRISTOPHER CLEOPHACE RUGEMALILA alikamatwa na alipopekuliwa alikutwa na Tsh 110,000,000/= USD 19,000 zikiwa ndani ya gari lake T 691 BMW DSU, Magari matano yenye namba za usajili, kama ifuatavyo;
  • T691DSU BMW yenye thamani yake Tsh 15,000,000/=
  • T909DSU Toyota Runx yenye thamani Tsh 13,000,000/=
  • T627DSU Toyota IST yenye thamani ya Tsh 11,000,000/=
  • T653DSU Toyota IST, yenye thamani ya Tsh 11,000,000/=
  • T857DSU Toyota IST. yenye thamani ya Tsh 11,000,000/=
Mtuhumiwa baada ya kuendelea kuhojiwa alikiri tayari ameshanunua nyumba mbili na kiwanja kimoja vyenye thamani ya TSH 107,000,000/= samani za ndani vyenye thamani ya Tsh 5,000,000/= na kufanya jumla ya mali na fedha taslimu Tsh 297,110,000/= USD 21,000.

Tarehe 21/02/202 watuhumiwa wawili walikamatwa MOHAMED RAMADHANI na SALIMU SHAMTE huko Mbagala na walipopekuliwa walikutwa na Tsh 332,000,000/= USD 50,000, EURO 5010 na GARI T134 DHY Toyota IST iliyotumika kubebea fedha baada ya kuiba na kutelekeza gari la kampuni ya G4S.

Watuhumiwa wote wawili baada ya mahojiano walikiri kununua viwanja viwanja viwili maeneo ya kisemvule na kivule vyenye thamani ya Tsh 25,000,000/=. Jumla kuu ya mali na fedha taslimu ni Tsh 357,000,000/=USD 50,000 na EURO 5010

Aidha upelelezi uliendelea na tarehe 24/02/2020 mtuhumiwa IBRAHIMU RAMADHANI MAUNGA alikamatwa na baada ya kupekuliwa alikutwa na Tsh 195,213,450, USD 70,600, nyumba aliyonunua kibaha Tsh 30,000,000/= na samani za ndani zenye thamani ya Tsh 10,000,000/=

Jumla kuu ya mali na fedha ni Tsh 253,000,000/=

Jeshi la polisi kanda maalum limefanikiwa kukamata watuhumiwa wote watatu pamoja na mtuhumiwa mmoja ambaye aliwasaidia kukamilisha wizi huo.

Sambamba na hilo, tunawashikilia askari Polisi tisa kwa kukiuka maadili ya kazi wakati wa ufutiliaji na upekuzi wa tukio
hili.

KUUWAWA KWA JAMBAZI SUGU JIJINI DSM
Katika tukio la pili, mnamo tarehe 24/02/2020 majira ya saa saba na nusu usiku huko maeneo ya saba saba mbagala kizuiani, kikosi kazi cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa RAMADHANI RASHIDI @ASNEY MJEURI (20) mkazi wa mbagala, mtuhumiwa huyo wakati mahojiano alikiri kujihusisha na tuhuma mbalimbali za ujambazi maeneo ya TOANGOMA, Mbagala na Mkuranga. Ndipo alikubali kwenda kuwaonyesha askari alipoficha silaha na watuhumiwa anaoshirikiana nao na walipofika eneo hilo alianza kukimbia huku akipiga kelele na askari walifyatua risasi tatu hewani kumuamuru asimame lakini mtuhumiwa huyo aliendelea kukimbia na ndipo alipopigwa risasi mgongoni na kufariki dunia.

LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR
ES SALAM.

25/02/2020

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa Kukutana na Watengenezaji wa GONGO ili Kuona Namna ya Kuiboresha

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema bado nia yake ya kukutana na Watengenezaji wa pombe aina ya gongo iko palepale

Amesema, lengo ni kujadiliana na kuona namna nzuri ya kuiboresha pombe hiyo kwa kuipelekea TBS na kwa Mkemia ili ipimwe na kuondoa sumu

Amesema, badala ya kuikuza na kuona kuwa hapa kuna kitu kinaweza kutupeleka kwenye viwanda, tunazuia. Je, mnaokunywa hizo pombe za viwandani mnajua asili yake?

Amehoji, "Kwanini gongo haitambuliwi kama kinywaji halisi cha Kitanzania?" Na kusisitiza kuwa atakutana na Watengenezaji wa gongo ili waone namna ya kuiboresha

Amesema “Nasisitiza nitakutana na watengenezaji wa gongo, kama unamfahamu mwambie aje tuzungumze jinsi ya kuiboresha zaidi na ituletee faida, hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda ya zuiazuia, tunapaswa kuwa na Tanzania ya Viwanda ya wezeshawezesha"

Itakumbukwa kuwa Katika Mkutano wa 11, Kikao cha 4 cha Bunge la Aprili 11, 2008, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge alisema yawezekana kabisa tuna pombe kali zaidi ya gongo, la msingi lililozingatiwa katika kupiga marufuku pombe aina ya gongo ni kwa sababu njia inayotumika kutengenezea si ambayo inazingatia usafi na afya ya binadamu, ndiyo maana imekuwa ni haramu kwa mujibu wa sheria.

Pale ambapo viwanda vya kutengeneza pombe ambayo inakubalika kwa masharti ya afya ya binafamu, vitakapoanza kutengeneza gongo, ndiyo hapo ambapo tutazingatia kuihalalisha pombe hiyo.

Mke wa Kobe Bryant aishitaki kampuni ya ndege iliyosababisha ajali ya mume wake

$
0
0
Vanessa Bryant ambaye ni mke wa  Kobe Bryant, ameishtaki kampuni ya Island Express na rubani wa helikopta iliyopata ajali na kusababisha kifo cha mume wake na mwanae Gianna lakini pia watu wengine 7.

Akiongea jana katika siku maalumu ya kutoa heshima za mwisho kwa wapendwa wao alisema hali ya hewa haikuwa salama kwa safari, na helikopta ilikuwa mbovu kwanini iliruhusiwa kufanya safari huku hali ya hewa haikuwa salama kwa safari, hali ya kuwa wahusika wanaelewa fika mazingira yapi hayafai kufanya safari na mazingira yapi yanafaa kwa safari Za Helkopta

Ametaka kulipwa fidia kwa kupoteza wapendwa wake kwani anaamini kuna uzembe ulifanyika.

Jerry Muro Arudi Yanga Rasmi

$
0
0
Uongozi wa Klabu ya Yanga, leo Februari 25, 2020 umezungumza na wanahabari baada ya timu hiyo kutoka  sare katika michezo yake minne ambayo imewafadhaisha mashabiki wake.

Aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Jerry Cornell Muro,  leo ameibuka makao makuu ya timu hiyo Mtgaa wa Jangwani, Kariakoo, na kuongea na wanahabari kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Gwambina FC Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam 
 
“Wana Yanga kesho twendeni uwanjani kwa uwingi.  Ujio wangu leo ni ujio maalumu ambao umenileta hapa kuja kuleta ‘password’.  

"Habari ya Yanga kupoteza michezo yake msahau,  kila kitu kimewekwa sawa.  Benchi la ufundi, kocha wachezaji mambo ni fresh.  

"Tumeongea na kocha tumekubaliana kuanzia kesho hatutaki ushindi wa magoli machache, tunataka ushindi wa magoli matatu, manne, nane na kuendelea.

“Matokeo hayo yanapatikanaje?   Anajua yeye maana ametoka Ulaya amekuja Tanzania kufundisha mpira, tunataka ushindi.  

"Nimeleta password tunajua tumehujumiwa sana kwenye mechi zetu,  wao walikuwa wanapita hapohapo na kuvuruga mipango yetu nasema hujuma sasa basi.”-Amesema

Mwalimu ahukumiwa miaka 3 jela na kulipa fidia Mil.10 kwa kumsababishia ulemavu mwanafunzi wake

$
0
0
Na Amiri kilagalila,Njombe
Mahakama ya wilaya ya Njombe imemhukumu mwalimu Focus Mbilinyi aliyekuwa akifundisha shule ya msingi Madeke hapo awali kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na kulipa fidia ya shilingi milioni kumi baada ya kumkuta na hatia ya kumpiga mwanafunzi wake na kumsababishia ulemavu wa kudumu.

Hukumu hiyo imetolewa na mahakama ya wilaya ya Njombe kupitia hakimu Ivran Msaki ambae amesema mahakama imesikiliza ushahidi wa pande zote mbili wa shauri namba 141 la mwaka 2019 na kujiridhisha pasina shaka kuwa mtuhumiwa Mwal. Focus Mbilinyi alitenda kosa hilo.

Hakimu Ivran Msaki amesema kwamba kupitia mashahidi watano upande wa mtoa mashtaka na kwa kuzingatia ushahidi wa madaktari wa hospital ya mhimbili kitengo cha mifupa MOI uliowasilishwa na daktari Silvery Mwesigye mahakamanai hapo mahakama imemtia hatiani mwalimu Focus Mbilinyi Kwa kuhusika na kosa hilo.

Mahakama imeeleza kuwa mwalimu Focus Mbilinyi alimuadhibu mwanafunzi Hosea Manga kwa  mtindo wa kumningi’iniza miguu ikiwa juu ya dirisha huku kichwa kikiwa chini hali iliyompelekea kuanguka na kuvunjika kwa visahani vya uti wa mgongo na kumsababishia ulemavu.

Shauri hilo limesimamiwa na mawakili watatu upande wa utetezi ambao ni Innocent Kibadu , Lilian Gama na Octavian Mbugwani huku upande wa serikali ukiwakilishwa  Wakili msomi na Elizabeth Malya na jumla ya mashahidi 8 wa pande zote mbili.

Kupitia kifungu cha sheria namba 235 kifungu kidogo cha cha 1 cha kanuni ya adhabu namba 20 mahakama imemtia hatiani mwalimu focus mbilinyi na kumhukumu kifungo cha miaka  mitatu jela na Kupitia kifungu cha sheria namba 348 kifungu kidogo cha cha kwanza cha kanuni ya adhabu namba 20 mahakama imemtaka mwalimu huyo kulipa fidia ya fedha kiasi cha Shilingi Milioni kumi kwa kumsababishia ulemavu mtoto Hosea Manga.

Ikumbukwe kwamba mwalimu Focus Mbilinyi anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo tarehe 21 mwezi March mwaka 2017 huko kijiji cha Madeke kilichopo wilaya na mkoa wa Njombe.

Hata hivyo mahakama imetoa nafasi ya siku thelathini kukata rufaa endapo upande wa utetezi haujaridhika na adhabu iliyotolewa.

Naibu Waziri wa Afya wa Iran Akumbwa na Virusi Vya Corona....16 Wafariki Dunia Kwa Virusi Hivyo Nchini Humo

$
0
0
Watu wawili walioambukizwa virusi vya Corona nchini Iran wamefariki, na kufikisha idadi ya waliofariki nchini humo kuwa watu 16, maafisa wamesema leo, wakati Wairan wakiwa na hofu kuwa huenda viongozi hawatilii maanani kiwango cha maambukizi. 

Iran ina idadi kubwa ya vifo kutokana na virusi vya Corona nje ya China, ambako virusi hivyo vilianzia mwishoni mwa mwaka 2019. 

Miongoni mwa wale walioambukizwa ni pamoja na naibu waziri wa afya, ambaye alipatikana kuwa ameambukizwa virusi hivyo vya Corona.

 Maambukizi mapya ya virusi vya Corona vimethibitishwa leo nchini Italia pamoja na Austria, Croatia na nchini Uhispania, masaa kadhaa kabla ya mkutano wa mawaziri wa afya wa Umoja wa Ulaya unaofanyika leo. 

Waziri mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic amesema nchi hiyo ina mgonjwa mmoja.

Idadi jumla ya wagonjwa nchini Italia imepanda hadi watu 283, ikiwa ni ongezeko la watu 54 kuanzia jana jioni.

Vijana Wenye Nia Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo Waahidiwa Kupewa Ardhi Songwe

$
0
0
Vijana wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya kilimo Mkoani Songwe wamepewa ahadi ya kupatiwa ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo ndani ya muda mfupi baada ya kuwasilisha maombi yao.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amtoa ahadi hiyo leo wakati akifunga Kongamano la Vijana  katika Kilimo lililofanyika Mkoa wa Songwe na Kuhusisha vijana takribani 700 kutoka Mikoa ya Songwe, Rukwa, Mbeya na Katavi.

Brig. Jen. Mwangela amesema Mkoa wa Songwe unayo ardhi ya kutosha kwa ajili ya shughuli za Kilimo ambayo bado haijatumika hivyo kijana yeyote mwenye nia ya kuwekeza katika Kilimo afike ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

“Mkoa una hekta Milioni mbili, mpaka sasa tumetumia asilimia 30 kwa ajili ya kilimo na asilimia ndogo kwa ajili ya makazi na misitu hivyo tunalo eneo la kutosha, mvua za kutosha na ardhi nzuri pia tunazo hekta elfu 18 zinazofaa kwa ajili ya kilimo cha umwgiliaji hivyo ardhi bado ipo ya kutosha.”, amesema Brig. Jen. Mwangela.

Ameongeza kuwa kijana mwenye nia ya kuwekeza kwenye Kilimo akifika ofisi ya Mkuu wa Mkoa ata taja Wilaya anayotaka kewekeza ili aelekezwe isipokuwa kijana hatatakiwa kuchagua mwenyewe eneo maalumu ambalo tayari linamilikiwa na watu wengine.

Brig. Jen. Mwangela amewasisitiza Vijana kuchangamkia fursa ya kumiliki ardhi kihalali kwakuwa bado inapatikana kwa urahisi ili baadaye wasihangaike kuitafuta wakati wa uzee na kuongeza kuwa waache kulalamikia wazazi au serikali kutokana na umasikini bali wajikite katika Kilimo.

Amesema asilimia 67 ya nguvu kazi ni vijana ambao hawana ajira ambapo nguvu kazi hii ikibaki bila ajira ni aibu kwa vijana na taifa hivyo mkakati wa Wizara ya Kilimo wa Kuhakikisha vijana wanajikita katika Kilimo ni mzuri na utainua uchumi wa taifa kwa haraka.

Brig. Jen. Mwangela ameongeza kuwa vijana wakishiriki kikamilifu katika Kilimo uchumi utakua, viwanda vitaongezeka na wataweza kuyafurahia maisha kwakuwa Kilimo hakijawahi kumtupa mtu na pia wasiache kuangalia fursa katika sekta za ufugaji na uvuvi.

Aidha Brig. Jen. Mwangela amewaeleza Vijana waliohudhuria Kongamano hilo kuwa Serikali itawaunganisha na taasisi zinazotoa mikopo ya Kilimo isipokuwa watatakiwa kuwa waamini na kurejesha mikopo hiyo.

Ameongeza kuwa wapo baadhi ya watu ambao walipatiwa mikopo ya Kilimo na baadhi ya benki lakini wamekuwa sio waaminifu kwa kutorudisha mikopo hiyo au kuwa wasumbufu katika kurejesha mikopo hiyo hivyo vijana hao wasiige mifano yao.

 Naye Afisa Programu kutoka Jukwa la Wadau wa Kilimo (ANSAF) Rehema Msami amesema wamefanya utafiti kuhusu namna ambayo halmashauri zimekuwa zikitoa asilimia 10 ya mapato yao kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu.

Msami amesema utafiti wao umebaini kuwa vijana wengi wenye sifa hawapati mikopo hiyo na hivyo kushindwa kuwa na mitaji ya kuwekeza katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo, pia baadhi ya vijana wanaopewa mikopo hawana sifa na hivyo kushindwa kurejesha mikopo hiyo.

Nelusigwe Kibona kijana Mkulima wa Mbogamboga kutoka Rungwe Mkoani Mbeya amesema Kongamano la Vijana limempa elimu na mbinu nyingi za Kulima kisasa pamoja na kutafuta masoko ya mazao yake.

Kibona ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Songwe kwa kuwasaidia vijana kupata ardhi kwa ajili ya Kilimo na kuiomba mikoa mingine iige mfano huo.

Kenedy Kyando Kijana Mkulima Kutoka Vwawa Songwe amesema kuwa Vijana wengi hawataki kujishughulisha na Kilimo kwa kukosa uvumilivu na kutaka fedha za haraka huku akiiomba Serikali kufanya makongamano kama hayo mara kwa mara.

Wachina Wawili Kortini Kwa Tuhuma Za Kutoa Rushwa Ya Tsh. Milioni 11.5 Kwa Kamishna Mkuu Wa TRA

$
0
0
Zheng Rongman na mkewe, Ou Ya wote raia wa China wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kutoa rushwa ya Dola 5,000 za Kimarekani sawa na Sh11.5 milioni kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania (TRA), Dk Edwin Mhede.

Rongman ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ronglan Intl Industry and Trade Co Ltd na mkewe wamekiri kutaka kutoa rushwa kwa bosi huyo wa TRA. Wanandoa hao ni  wakazi wa Wilaya ya Mafinga mkoani Iringa.

Wamefikishwa mahakamani leo Jumanne Februari 25, 2020  na kusomewa shtaka moja la kutoa rushwa.

Baada ya kusomewa shtaka lao, walikiri kutenda kosa hilo na
Hakimu Shaidi amesema kesi hiyo itaendelea kesho kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 26, 2020 itakapoendelea na washtakiwa wamerudishwa rumande.

==>>Msikilize Hapo Chini
_______________





.

Mume amuua Mkewe kwa kumchoma na mkuki mgogongoni ukatokea kwenye titi Upande wa Kushoto

$
0
0
Jeshi la polisi Mkoa wa Tabora linamshikilia Omary Dweka maarufu  "Mkuyu" kwa tuhuma za kumvizia na kumuua Mkewe Hawa Juma (35) kwa kumchona mkuki mgongoni na kutokea upande wa mbele ya ziwa la kushoto. 

Akizungumza leo Jumanne Februari 25 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika kijiji hicho kilichopo barabara kuu ya kuelekea Wilaya ya Nzega.

Amebainisha kuwa alimchoma mkuki mgongoni na kutokea kifuani upande wa kushoto na alifanya kitendo hicho wakati mkewe amelala.

“Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani muda wowote kwani upelelezi umekamilika,” amesema Kamanda Mwakalukwa akibainisha chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano February 26

Chelsea Yachezea Kichapo cha 3-0 Toka Kwa Bayern Munich

$
0
0
Mechi kati ya Chelsea na Bayern Munich iliwashuhudia wababe wa Bundesliga wakipiga hatua kubwa ya kukaribia kufuzu kwa duru ya nane bora ya Ligi ya Mabinwa baada ya kushinda  3-0 uwanjani Stamford Bridge.

Matokeo ya kuridhisha katika awamu ya pili siku ya Jumanne, Februari 25 usiku, yalichochewa na Robert Lewandowski ambaye alisadia Bayern kutwaa ushindi.
 
Upande zote zilionyesha umahiri katika awamu ya kwanza na kutoka sare tasa kuelekea muda wa mapumziko, huku Thomas Muller akikaribia kuvunja kimya baada ya kupiga shuti iliyotua juu ya lango.

Lewandowski pia alinyimwa nafasi mara mbili na Willy Caballero kufunga bao, huku juhudi za Marcos Alonso dakika ya 41 ikizua hatari kwa Chelsea.

Katika kipindi cha pili, wenyeji walionyesha ari ya kuwa kifua mbele huku Manuel Neur akilazimika kupangua mikiki ya Mason Mount na Ross Barkley.

Hata hivyo, Bavarians walifunga bao la kwanza kupitia kwa Serge Gnabry ambaye alivurumisha kombora lililotua kimyani baada ya kuwasiliana na Lewandowski.

Gnabry alisawazisha bao hilo dakika tatu baadaye kufuatia usaidizi wa Lewandowski, kabla ya fowadi huyo kuingia katIka orodha ya watingaji bao dakika ya 76 na kuzima ndoto ya Chelsea.

Matumaini ya wenyeji kupata bao la kufutia machozi ilididimia kunako dakika ya 84 baada ya Alonso kutimuliwa uwanjani kwa kumuangusha Lewandowski.

Masogora wa Frank Lampard kwa sasa wana kibarua kigumu cha kubatilisha matoke hayo wakati wa ziara yao ya Ujerumani kwa mechi ya marudiano ili kufuzu kwa raundi nyingine ya kivumbi hicho cha Uropa.

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>