Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Nafasi za Kazi 92 TANESCO...Mwisho wa Kutuma Maombi ni March 1, 2020

$
0
0

QUALIFICATION AND EXPERIENCE

Form IV and/or VI Secondary School Academic Certificates with Electrical Installation Trade Test Level II and III. Valid Driving License Class C, C1, C2, C3 and/or E will be an added advantage.
_________________________


QUALIFICATION AND EXPERIENCE

• Form IV and/or VI Secondary School Academic Certificates with Basic and/or Professional Driving Certificate from National Institute of Transport (NIT) & and/or VETA;
• Valid Driving License Class C/C1/C2/C3 and/or E;
• Trade Test Grade II or III I in Automobile Engineering/Mechanics from recognized institution is an added advantage;
__________________________


QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Bachelor Degree either in Marketing, Business Administration (majoring in Marketing or Public Relations) or Mass Communication and Public Relations from recognized Institution; Computer knowledge is compulsory; and relevant working experience of one (1) year in a reputable organization.
_____________________


QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Ordinary Diploma in Electrical Engineering from recognized institution. A driving license class C, C1, C2 and E will be an added advantage. 
_____________________ 

==>>Kwa Nafasi Zingine Nyingi Zikiwemo za Mabenk, Makampuni Binafsi <<BOFYA HAPA>>


Watumishi Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Watakiwa Kutunza Siri

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima amewataka watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufanya kazi kwa kushirikiana, uwajibikaji na kutunza siri za ofisi kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi Tawi la NIDA, Kailima alisema mafanikio ya Mamlaka hiyo ni pamoja na kushirikiana katika utendaji wa kazi ili kuleta weledi, na pia kuepuka kutoa siri za ofisi kwa mujibu wa utaratibu wa utumishi wa umma.

Pia aliwakumbusha watumishi hao kutoka Makao Makuu ya NIDA na Ofisi zake Mikoani, kuhakikisha uwajibikaji unakuwepo kwa upande wa mwajiri na mwajiriwa kwa kufanyiwa kazi kile kinachotakiwa kufanyiwa kazi na kisichohitajika kuifanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.

“Tukoseane kwa nia ya kuboresha, tusikoseane kwa nia ya kubomoa kwa sababu ya kupata fursa hii ya kuwa na haki na hadhi sawa, na pande zote mbili ziwajibike kuwajibishana,” alisema Kailima.

Aliongeza kuwa, watumishi wanapaswa kupewa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mamlaka na masuala yanayowahusu kwa utaratibu wa ofisi au unaoidhinishwa na Mkurugenzi Mkuu na si vinginevyo.

“Muhakikishe mnatoa huduma kwa wananchi sehemu zote nchini kwa weledi, maafisa wafike mapema katika maeneo ya kazi na kutoa vitambulisho vya Taifa mapema, na wananchi waridhike na huduma hiyo mnayoitoa, kwa hatua hiyo mtapunguza malalamiko ya wananchi,” alisema Kailima.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Arnold Kihaule alitoa mafanikio ya Mamlaka yake hadi kufikia Desemba mwaka 2019, alisema NIDA imefanikiwa kusajili wananchi 21,511,321, Wageni wakaazi, 19,311 na Wakimbizi 274,000 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

“Pia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imezalisha namba za utambulisho 16,211,654 na kutoa vitambulisho 5,787,869, na vimewafikia wananchi ilipofika mwezi Desemba 2019,” alisema Dkt. Kihaule.

Kikao cha Baraza hilo cha siku moja pia kilipitia Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2019/20 kwa Kipindi cha kwanza cha Mwezi Julai hadi Desemba na Makadirio ya Bajeti ya Mamlaka kwa Mwaka wa Fedha 2020/21.

Madalali Na Waendesha Minada Wasiofuata Sheria Kukiona Cha Moto

$
0
0
Na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James mewaonya madadali na waendesha minada Tanzania Bara kuacha mara moja kufanya biashara hiyo bilaa kujisajili kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Bw. James ametoa onyo hilo Jijini Dar es Salaam wakati akizundua Mfumo Mpya wa Kieletroniki wa utoaji leseni za udalali na uendeshaji wa minada ya hadhara Tanzania Bara ambapo watoa huduma hiyo kuanza sasa wanatakiwa kujisajili kupitia mfumo huo kwa njia ya mtandao wa Internet ama kupitia simu zao za kiganjani.

‘’Napenda kuwafikishia taarifa hii wananchi wote, hasa Madalali na waendesha minada, kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kufuatilia na kuchukua hatua kali kwa wote watakaojuhusisha na shughuli za udalali na uendeshaji wa minada bila kuwa na leseni halali’’ alisema Bw. James.

Aliziagiza Taasisi zote za Serikali kufanya kazi na Madalali na waendesha minada ambao wanatambulika kisheria na kwa kufanya hivyo watakuwa wameisaidia Serikali kujipatia mapato yatakayotokana na ada ya leseni itakayolipwa na wafanyabiashara ya udali na waendesha minada.

“Mfumo huu utapunguza changamoto zilizokuwepo hapo awali ambazo zilikuwa zinatumia mlolongo mrefu wa kupata leseni kwa kuwa mfumo huo  umeunganishwa na Mfumo wa Malipo wa GePG ambapo mwombaji ataweza kulipia ada ya leseni kwa kutumia benki, mawakala au simu za kiganjani na hivyo kurahisisha na kuboresha ulipaji, kupunguza gharama za ulipaji na kuongeza uwazi na udhibiti wa Fedha za Umma.

Bw. James aliutangazia Umma kuwa kuanzia  tarehe 24 Februari, 2020 maombi yote ya leseni za Udalali na Uendeshaji wa Minada Tanzania Bara yawasilishwe kupitia Mfumo wa Utoaji wa Leseni za Udalali na Uendeshaji Minada ambao unapatikana katika tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango (www.mof.go.tz);

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. Chotto Sendo, amesema biashara ya udalali na uendeshaji wa minada hapa nchini imekuwa ikikua kwa kasi na hivyo kutengeneza ajira, kuongeza kipato pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Bw. Chotto aliongeza kuwa leseni za Udalali na uendeshaji wa minada Tanzania Bara zinatolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa mujibu wa sheria ya waendesha minada ya Mwaka 1928 iliyorejewa Mwaka 2002, na Wizara imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kutatua changamoto zinazowakabili wadau hawa ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Wakizungumza kwa niaba ya madalali, Mwenyekiti wa Chama cha Mdalali wa Mahakama Bi. Mwamvua Kigulu na Mwenyekiti wa madalali Binafsi Bw. Phidel Katundu, wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kubuni mfumo huo utakao wapunguzia gharama ya kufuata huduma ya usajili jijini Dodoma.

Wameiomba Serikali kudhibiti madalali wasio na leseni au wale wasiosajiliwa kwa kuwa wanaikosesha Serikali mapato pamoja na kuchafua taswira ya biashara ya udalali nchini.

Wamemwomba Katibu Mkuu Bw. Doto James kupitia upya Sheria ya Udalali ya Mwaka 1928 ambayo wamesema imepitwa na wakati na inakwaza shughuli za udalali nchini ikiwemo urasimu wa ufanyakazi kazi zao kutoka kwa mamlaka za Serikali Kuu hasa makatibu Tawala wa Wilaya ambao wanataka kupata vibali kutoka kwao kabla ya kutekeleza kazi zao za udalali katika maeneo husika.
 
MWISHO

Vifo Vya Wajawazito Kipindi Cha Kujifungua Vyapungua Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Temeke

$
0
0
Na. Catherine Sungura - Dar es Salaam
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa temeke imejipanga kuokoa maisha ya wakina mama, wajawazito hususan katika kipindi cha kujifungua, kutimiza lengo hilo imeboresha miundombinu yake, vifaa tiba pamoja na kuimarisha huduma za afya kwenye ngazi za msingi.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati wa ziara yake ya kikazi hospitalini hapo, ambako alikwenda kwa lengo la kusikiliza maoni na changamoto kutoka kwa wananchi na watumishi wa hospitali hiyo.

“Mwaka 2018 walikuwa na vifo 19 vya wajawazito na 2019 walikuwa na vifo 8 tu, lakini kwa takwimu za kuanzia Novemba 2019 hadi leo hakuna mwanamke mjamzito aliyekuja hospitalini hapa na kupoteza maisha, niwapongeze madaktari, wauguzi na watoa huduma wote wa hapa kwa hatua hii," amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa jitihada za makusudi, kuwekeza kwenye huduma za afya nchini sambamba na ujenzi wa vituo vya afya na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa.

“Sasa hivi hapa temeke kuna huduma za kibingwa za meno ambapo zamani haikuwepo," amesema.

Waziri Ummy amesisitiza Wizara ina mpango pia wa kuhakikisha huduma zote za kibingwa zinazohitajika zinakuwepo kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa.

Hata hivyo amesema kuwa wanawake 15 kati ya wanawake 100 ndio ambao huhitaji kupelekwa kujifungulia kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa hususan wale wenye changamoto za ujauzito, kwa mfano mtoto amekaa vibaya au viashiria vya uzazi pingamizi.

Kwa upande  wa vipimo waziri huyo amesema kuwa Wizara yake imeongeza vipimo vya utra sound hivi sasa serikali imeboresha vituo vya afya na kwamba vipimo hivyo vinaanza kutolewa kuanzia ngazi za vituo vya afya vya umma na hospitali za wilaya nchini.

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma kuanzia ngazi ya msingi na hospitali za rufaa za mikoa ni kwa wagonjwa watakaopata rufaa.

“Kwa yeyeote atakayefanya makusudi kukorofisha vipimo ili watu waende kupima kwenye vutuo binafsi tutawachukulia hatua kwani ni wahujumu uchumi, tunataka vipimo vyote vifanyike ndani ya hospitali ila pale mashine haipo tutaruhusu, lengo letu ni kujitosheleza kwa vipimo vyote kwenye vituo vya afya vya umma," amesisitiza Waziri Ummy.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Yudas Ndungile amesema kuwa kutokana na maboresho ya miundombinu, wataalam na vifaa tiba kwa mkoa huu wameweza kupunguza vifo vipatavyo arobaini kwa mwaka ukilinganisha na vifo186 mwaka 2018 hadi vifo 140 mwaka 2019 na matarajio yao ni kupunguza zaidi.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt. Meshack Shimwela amesema kuwa  hospitali hiyo imeondoa msongamano wa wajawazito kwa kuwa hivi sasa wananchi wengi wanafuata mfumo wa rufaa.

"Hivyo wakina mama wajawazito wanaofika kwenye hospitali hii ni wale wenye changamoto ya uzazi kwa maana hiyo wengi wanajifungulia kwenye ngazi za chini ambapo huduma za afya nazo zimeboreshwa," amesema.

MWISHO

Majadiliano Sekta ya Umma na Binafsi Chachu Ukuaji wa Uchumi

$
0
0
Na Jacquiiline Mrisho – MAELEZO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema kuwa majadiliano ya mabaraza ya biashara yanayofanyika katika ngazi ya Taifa, Mikoa na Wilaya yameendelea kusaidia uchumi wa nchi kuimarika.
 
Waziri Mhagama ameyazungumza hayo leo Jijini Dodoma wakati akizindua Muongozo wa majadiliano kati ya sekta ya Umma na Binafsi katika ngazi ya Mikoa na Wilaya uliofanyika jijini humo ambapo amesema kuwa inawezekana mabaraza ya biashara  yalikuwa hayafanyiki vizuri kwa sababu watu walikuwa wanashindwa kutumia mazingira waliyonayo kujipanga kuendesha mabaraza haya lakini, muongozo huo utasaidia watu kukutana kwa ajili ya majadiliano yenye tija.  
 
“Ili kuwa na utendaji unaotukuka lazima tuwe na muongozo wa nini kifanyike, wakati gani, kwa utaratibu upi na kwa rasilimali zipi, hatuwezi kuzungumza uchumi wa viwanda wala utekelezaji wa Dira ya Maendeleo bila sekta binafsi hivyo kuna kila haja ya kutengeneza mazingira wezeshi yatakayoifanya sekta ya umma isaidiane na ishirikiane kwa karibu na sekta binafsi ili yaliyopangwa yaweze kutekelezwa”, alisema Waziri Mhagama.
 
Waziri Mhagama amesisitiza wahusika kutoa mrejesho wa majadiliano ya mabaraza ya biashara katika ngazi za mikoa na wilaya kwani kama yatafanyika maamuzi na kujiwekea malengo ambayo hayatekelezeki hakutakuwa na maana ya vikao hivyo.
 
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amesema kuwa muongozo huo ni kitendea kazi katika ngazi zetu za mikoa na wilaya kitakachowezesha uendeshaji wa mabaraza haya ambayo kwa kiasi kikubwa yataleta tija.
 
“Takwimu zinaonesha kuwa kati ya Mikoa 26 ni mikoa 16 pekee ambayo ilifanya mabaraza hayo, sasa muongozo umeshatolewa hivyo miongoni mwa taarifa za wakuu wa Mikoa zinazoletwa TAMISEMI lazima taarifa ya Uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara  katika mikoa yenu iwepo”, alisema Waziri Jafo.
 
Vile vile, Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa, Dkt. Godwill Wanga amesema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara kupitia majadiliano kati ya sekta hizo mbili ambapo inasimamia kwa karibu majadiliano hayo kama njia muafaka ya kufikia maridhiano yatakayoboresha uchumi na maendeleo endelevu ya nchi.
 
“TNBC tunatoa wito kwa wadau wote kutumia majadiliano haya kuainisha matatizo ya miradi ya pamoja kati ya sekta hizi mbili inayolenga kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini”, alisema Dkt. Wanga. 
 
Akiishkuru Serikali ya Awamu ya Tano, Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPFS), Rehema Mbogi amesema kuwa Serikali imeonesha umakini katika masuala yanayohusu majadiliano kati ya Sekta Binafsi na Umma katika ngazi zote kwani sekta binafsi imekua ikishirikishwa katika mabaraza ya biashara pamoja na kupata nafasi za kujadiliana masuala mbalimbali viongozi wa Serikali.
 
“Mnamo mwaka juzi nilishiriki katika mkutano nchini Afrika Kusini uliohusu mfumo wa majadiliano katika nchi za Kusini mwa Afrika nilifurahishwa kuona kwamba nimesimamishwa kuelezwa kwamba nchi yetu Tanzania ina mfumo bora wa majadiliano unaoeleweka kuanzia ngazi ya Taifa hivyo hii ni fursa nzuri ambayo tukiitumia vizuri tunaweza kufika mbali katika nchi”, alisema Bi.Rehema.

Jamii Yatakiwa Kutumia Fursa Ya Kilimo Ili Kujikwamua Kimaendeleo

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jamii imetakiwa kutumia fursa ya kilimo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kuondokana na upungufu wa chakula katika maeneo mbalimbali nchini kwa kutumia fursa ya mvua zinazoendelea kunyesha badala ya kulalamika kuwa maisha ni magumu.

Hayo yamesemwa na mtaalamu wa masuala ya kilimo AMBAYE kwa sasa anajishughulisha na uzalishaji wa mbegu za mazao mbalimbali  ikiwemo karanga na mtama jijini Dodoma 

ITHAN CHAULA amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitafsiri kilimo kama shughuli ambayo hufanywa na watu wa vijijini akiongeza kuwa sekta hiyo inapaswa kuheshimiwa, kuboreshwa kutoka kilimo cha jembe la mkono na kuwa kilimo cha kisasa.

Amebainisha kuwa  bado wakulima wanahitaji elimu  ya kilimo salama kukabiliana na changamoto ambazo hujitokeza  kama vile sumukuvu wakati wa kupanda, kuvuna na kuhifadhi akiomba serikali kupitia maafisa ugani kutembelea wakulima hasa maeneo ya vijijini kuwapa elimu na mbinu za kilimo bora chenye tija kuachana   na kilimo cha mazoea.

Chaula amewahimiza wakulima hasa mkoa wa dodoma kutumia vizuri utabiri wa hali ya hewa  ambao umekuwa ukitolewa kupanda mazao ambayo yanaweza kuhimili kujipatia chakula na kuyauza kujipatia kipato.

Aidha amepongeza serikali kwa juhudi inazofanya kuhakikisha mkulima anapatiwa mbegu akiiomba kurahisisha mchakato wa upatikanaji wa mbegu hizo  kwa bei rafiki na kwa wakati kumuwezesha mkulima kuendana na msimu
husika.

Jeshi La Polisi Dodoma Lamuita mwanaharakati Cyprian Musiba Kwa Mahojiano Kuhusu Tuhuma za Kutaka Kuuawa

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limemuita kwa mahojiano mwanaharakati huru Cyprian Musiba  baada ya kutoa tuhuma mbalimbali za kutishiwa kuuawa

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Feb.24.2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema Musiba kupitia baadhi ya magazeti hapa nchini amechapisha taarifa za kulalamika kutishiwa kuuawa  na baadhi ya wanasiasa .

Hivyo Kamanda Muroto ametoa Rai  kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa habari za makosa ya jinai kwenye vyombo vya habari bila kujulisha vyombo vya dola na jeshi hilo limemuita  Musiba kwa Mahojiano zaidi dhidi ya Malalamiko yake.

Katibu Mkuu CCM Dk Bashiru Ally Asema Hatima ya Makatibu Wakuu Wastaafu Adbulrahman Kinana , Yusuph Makamba na Benard Membe Itajulikana Wiki Hii

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
RIPOTI kuhusu tuhuma zinazowakabili makatibu wakuu wastaafu wawili(Adbulrahman Kinana na Yusuph Makamba) akiwemo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe tayari imekamilika na inatarajiwa kukabidhiwa kwa Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi mwishoni mwa wiki hii na kamati ndogo ya nidhamu chini ya uongozi wa Makamu Mwenyekiti wa chama, Bara Philip Mangula.

Kauli hiyo ilitolewa jijini hapa jana na Katibu Mkuu wa chama, Dk Bashiru Ally wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala matatu yakiwemo kuanza kwa vikao vya kamati kuu ya chama mwishoni mwa wiki, ziara ya siku tatu mkoani Mtwara na ugeni wa wanachama wapya kujiunga CCM.

Dk. Bashiru alisema kuwa siku saba zilizotolewa na kamati kuu ya chama zimeshamalizika ambapo taarifa hiyo itapitiwa kesho kutwa na kamati ndogo ya nidhamu ya chama ili iwasilishwe kwa kamati kuu mwishoni mwa wiki.

“Kamati kuu itakaa mwishoni mwa wiki hii ili kupokea taarifa ya Mangula hivyo wiki hii wakati vikao vikianza kamati hizo mbili kuu na ndogo ya nidhamu na maadili zitakaa,”alisema Dk. Bashiru.

Alifafanua kuwa uamuzi wa  chama ni kuwa taarifa ya Mangula ipo tayari kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye vikao vya chama ambapo baada ya vikao Polepole atatangaza kama wamebainika kuwa na makosa na hatua gani zitachukuliwa na kwa adhabu gani.

Alisema yapo makossa mengine ukithibitika adhabu yake haitangazwi na baadala yake anaambiwa mhusika na kwamba saa nyingine inaweza ikatolewa adhabu ya onyo kali hiyo itatangazwa hadharani.Pia unaweza kukosa aina fulani ya haki zako za uanachama .

“Ukithibitika umefanya makosa ya kukiuka kanuni hiyo mtu mwingine anakosa haki za uanachama na kuwa chini ya uangalizi.. lakini wakati mwingine mtu anapewa karipio kuliko onyo kali kama utaratibu wa kulitumikia ana muda wa uangalizi ili ajirekebishe,”

Alifafanua wakati mwingine hupelekea mhusika kuachishwa uanachama na kuwa raia huru lakini anaweza kujiunga tena na kujiunga kwa mujibu wa taratibu za kikanuni na kama ni kiongozi anaweza kusimamishwa uongozi kwa muda au kuachishwa.

Alifafanua kuwa adhabu hizo hutolewa baada ya watuhumiwa kusikilizwa, kujitetetea na baada ya kamati kuu kuchambua na kujiridhisha ili kutoa uamuamuzi.

“Kwa hiyo kuhusu hatua zitakazochukuliwa ni baada ya vikao vya kamati kukaa na kupokea taarifa ndio uamuzi utatolewa, hivyo taarifa ya Mzee Mangula itawasilishwa ndani ya kamati kuu mwisho wa wiki hii,”alisema.

Aidha, Dk. Bashiru amekanusha taarifa zilizosambazwa mtandaoni na baadhi ya watu kuhusu ziara yake mkoani Mtwara kuwa alikuwa akilindwa na askari polisi si za kweli.

“Kuna watu wameshaharibu sifa ya ziara yangu wametengeneza picha inayoonyesha gari la rangi ya kijani wanayoiita ya katibu mkuu halafu imezungukwa na polisi akaandika umoja wa vijana wakimlinda katibu mkuu wa CCM.

"Zipo mamlaka zinazoweza kusimamia matumizi bora ya mtandao nakanusha maana ziara yangu ilifanyika mchana na waandishi wa habari ni mashahidi hivyo tusaidiane kueleza kama ni kweli tulilindwa na viongozi wa dola,”alisema.

Aliongeza: "sio ziara yangu ya kwanza kufanyika mara nyingi huwa Napata ulinzi wa askari wa barabarani ni wa kawaida sina sababu ya kulindwa maana vyombo hivyo vinafanya kazi kwa mujibu wa sheria.

"Wana CCM tutumie vizuri mitandao ya kijamii nimemwelekeza Polepole aeleze sio gari la Katibu Mkuu na ziara ya Mtwara haikuwa hivyo na vyombo husika chukueni hatua."

Rais Magufuli Akutana na Profesa Lumumba..... Kansela wa Ujerumani amtumia ujumbe

$
0
0
Rais wa Tanzania, John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Msomi na Mwanajumui wa Afrika (Pan-Africanist) Profesa Patrick Lumumba, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli na Profesa Lumumba ambaye ni raia wa Kenya wamezungumzia masuala mbalimbali yahusuyo juhudi za Afrika katika kuimarisha uchumi kwa kutumia rasilimali zake .

Pia wajibu wa Waafrika na viongozi wao katika kuimarisha huduma za kijamii na kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Rais Magufuli amempongeza Profesa Lumumba kwa juhudi zake za kueleza waziwazi makosa yanayosababisha nchi za Afrika kubaki nyuma kiuchumi, kijamii na kisiasa, wajibu wa viongozi na wananchi wa Afrika katika kukabiliana na changamoto zinazozikabili nchi zao na mapenzi yake makubwa kwa Afrika.

Rais Magufuli amemueleza juhudi ambazo Serikali inazifanya katika kujenga uchumi imara wa kujitegemea ikiwamo utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa Bwawa la Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 za umeme na  kuongeza usambazaji wa umeme kutoka vijiji 2,018 hadi kufikia vijiji 8,587.

Pia, ujenzi wa barabara na madaraja makubwa na  madogo, kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari, kuongeza mikopo ya elimu ya juu, kuongeza ukusanyaji wa mapato, kudhibiti rasilimali muhimu ya madini na kupambana na rushwa.

“Mimi sijawahi kukutana nawe kabla, lakini nakusikia na kukuona kupitia vyombo vya habari jinsi unavyopaza sauti kuhusu Bara la Afrika, nakupongeza kwa juhudi hizo, na ninafarijika kwamba unaisemea vizuri Afrika,” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake, Profesa Lumumba amemshukuru Rais Magufuli kwa kutenga muda wake kuzungumza naye na amempongeza kwa juhudi kubwa alizozionesha katika kipindi kifupi cha uongozi wake wa miaka minne ambapo ameonyesha mfano wa namna ya kupigania rasilimali za nchi ikiwemo madini, kujenga nidhamu ya utumishi Serikalini, kuimarisha uchumi, kupambana na wizi wa mali za umma, rushwa na ufisadi.

Profesa Lumumba amesema inafaa kwa nchi za Afrika kujifunza mambo yanayofanyika Tanzania kwa sasa na amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Waafrika kujiamini na kuchukua hatua madhubuti za kuwaondoa katika hali ya sasa ambapo rasilimali zake zinachukuliwa na Mataifa ya nje ilihali wananchi wake wakikabiliwa na changamoto mbalimbali.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na Mwakilishi wa Kansela wa Ujerumani anayeshughulikia masuala ya Afrika, Guenter Nooke, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Nooke amewasilisha ujumbe wa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na pia ameelezea kufurahishwa kwake na hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa hapa nchini ikilinganishwa na alipokuja miaka iliyopita.

Pia amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali katika kupambana na rushwa na kuimarisha uchumi ambapo ameahidi kuwa Ujerumani itaendelea kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji na biashara na masuala mengine ya kijamii.

Kwa upande wake, Rais Magufuli amemhakikishia Kansela wa Ujerumani kuwa Serikali ipo tayari kuuendeleza na kuukuza zaidi uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati yake na Ujerumani, na inawakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kuja kuwekeza hapa nchini.

Katika mazungumzo hayo, Nooke ameongoza na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Regine Hess.

Mkataba Mpya Wa Ushirikiano Kati Ya Tanzania Na EU Uimarishe Sekta Za Maendeleo

$
0
0
Na. Peter Haule na Josephine Majula, WFM, Dodoma
Serikali imeuomba Umoja wa Ulaya (EU) kuwekeza katika maeneo ya maendeleo ambayo tayari Serikali imeanza kuyatekeleza ikiwemo uboreshaji wa miundombinu katika mkataba mpya wa ushirikiano kati ya Tanzania na EU kwa mwaka 2021 hadi 2027.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi.

Dkt. Mpango alisema kuwa, katika mkataba mpya wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na EU unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2021 ni vema ukaendelea kuimarisha maeneo ya maendeleo ambayo tayari yameanza kutekelezwa na Serikali hususani katika Sekta ya Elimu, Afya, miundombinu na mingine ili kufikia malengo endelevu.

“Tuna kazi kubwa ya kuwekeza kwenye rasilimali watu kwa kuwa miradi kama miundombinu haiwezi kufikia malengo yake bila kuwa na uwekezaji katika rasilimali hiyo na ndio maana kama Serikali tumeamua kutoa elimu bure kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari”, alieleza Dkt. Mpango.

Alisema kuwa katika suala la miundombinu, Serikali inaangalia uwezekano wa kuanza ujenzi wa Reli kutoka Bandari ya Mtwara katika Bahari ya Hindi hadi Bandari ya Mbamba Bay katika Ziwa Nyasa, ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na kuokoa fedha nyingi zinazotumika kukarabati barabara zinazoharibika kwa usafirishaji wa bidhaa kwa njia ya barabara.

Aidha alieleza kuwa miundombinu hiyo ya reli itakuwa na matawi kuelekea Liganga ambako kunapatikana madini ya Chuma na Mchuchuma ambako kuna hazina kubwa ya Makaa ya Mawe.

Alisema Reli hiyo itasaidia pia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kwenda nchi jirani ikiwemo Malawi, hivyo kuchochoa biashara na kuongeza mapato.

Kwa upande wake Balozi wa EU nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, aliipongeza Serikali kwa kuwa na Sera nzuri za maendeleo lakini pia akasema kuwa ili kuboresha mazingira ya kibiashara, miongoni mwa mambo yanayohitajika ni pamoja na Miundombinu, mafunzo, kuwa na uchumi wa kidigitali na siasa bora, mambo ambayo Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuyatekeleza.

Mkataba wa ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi uliokuwa ukitekelezwa kuanzia mwaka 2014 unamalizika mwaka huu ilihali kwa sasa kunatarajiwa kuwepo kwa majadiliano ya mkataba mwingine wa ushirikiano unatarajia kuanza kutekelezwa mwaka 2021 na kumalizika 2027.

Katika tukio jingine, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango namekutana na mkufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikianao wa Biashara wa Finland, Mhe.  Ville Skinnari, ambapo walijadili mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya ushirikiano na maendeleo ya kiuchumi.

Mwisho

Hukumu Ya Kesi Ya Uchochezi Inayowakabili Viongozi Chadema Kutolewa Machi 10, 2020

$
0
0
Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Machi 10, mwaka huu kutoa hukumu ya kesi ya uchochezi dhudi ya viongozi nane wa Chadema akiwemo  Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho,Dk.Vicent Mashinji ambaye hivi karibuni  amehamia CCM. 

 Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amesema sheria inaelekeza pande zote kufanya majumuisho ili kuisaidia mahakama kutoa uamuzi kwa kuangalia masuala ya kisheria yaliyoibuliwa wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo na wametoa maelekezo kwa pande hizo kuwasilisha hoja zao katika siku tano za kazi baada ya mahakama kukamilisha uchapaji wa nyaraka zilizopo kwenye kesi hiyo na kuwapatia.

Amesema, anatambua kesi hiyo inamvuto kwa jamii, hivyo ni lazima iishe ili kila mmoja aweze kuendelea na shughuli zake na kuongeza  "Majumuisho ya mwisho mnatakiwa muyawasilishe siku tano za kazi," amesema Hakimu Simba. 


Ameongeza kesi hiyo inakurasa zaidi ya 1,000 ambazo anatakiwa kuzipitia na kutoa hukumu hivyo hukumu ya kesi hiyo itatolewa Machi 10, mwaka huu saa 4:30 asubuhi. 

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Naibu Katibu mkuu wa Chadema upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu,  Katibu Mkuu Chadema na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Jumla ya mashahidi nane wa upande wa mashtaka walifika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao ambapo mahakama iliwaona washitakiwa wote kuwa na kesi ya kujibu na walijitetea kwa kuleta mashahidi kumi na tatu. 

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

Wizara Ya Kilimo Kutumia Vijana Kuendeleza Kilimo Nchini

$
0
0
Wizara ya Kilimo imeanzisha Mpango wa kutumia Vijana katika kuendeleza sekta ya Kilimo Nchini kwakuwa wao ni nguvu kazi ambayo inaweza kuleta mabadiliko ya haraka.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameyasema hayo mapema leo wakati akizindua Kongamano la Vijana katika Kilimo lililozinduliwa kitaifa Mkoani Songwe na kushirikisha Vijana kutoka Mikoa ya Songwe, Mbeya, Rukwa na Katavi.

“Wizara ilifanya tathmini na kuona kuwa licha ya mambo mazuri tunayofanya, inabidi katika mikakati yetu tuwe na Mkakati wa Kuwatumia Vijana ili waingie katika Kilimo.”, amesema Waziri Hasunga.

Ameongeza kuwa ili kufanikisha Mpango huo Wizara ya Kilimo itahakikisha ardhi inayofaa kwa Kilimo inapatikana na Kutengwa kwa kuwa na sheria ya kutenga ardhi ya Kilimo, pia Mikoa inapaswa kutenga maeneo yanayo faa kwa ajili ya Kilimo.

Waziri Hasunga amesema Wizara pia itahakikisha upatikanaji wa rasilimali fedha, pembejeo na zana za Kilimo, Miundombinu ya Umwagiliaji inawekwa kwakuwa Mvua ikizidi au kupungua ni hasara kwa Mkulima pamoja na kufundisha mbinu na ujuzi wa ujasiriamali katika kilimo kupitia Makongamano.

Amesema Wizara inatambua kuwa Vijana ndio nguvu kazi huku takwimu zikionyesha kuwa asilimia 96 ya watanzania hawaja ajira hivyo, hiyo ni nguvu kazi ambayo inatakiwa ielekezwe katika Kilimo.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa Wizara ina tambua changamoto zilizopo katika sekta ya Kilimo na tayari imechukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kuanzisha utaratibu wa kusajili wakulima ili watambulike kwa urahisi, kusajili waadau wa Kilimo na Kuanzisha Bima ya Mazao.

Aidha amewataka vijana wote kubadili mtazamo kuwa kilimo ni kushika jembe la Mkono kwakuwa Kilimo ni sekta pana inayojumuisha kulima, kusindika na kuongeza thamani ya mazao, masoko, uhifadhi na pembejeo hivyo wasiache kujikita hata katika moja ya fursa hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amesema Mkoa wa Songwe  ni moja kati ya wazalishaji wakubwa wa Chakula Nchini ambapo uzalishaji unafanyika ajili ya Chakula na Kuuza ndani na nje ya nchi pia uhakika wa kuvuna kwa wingi chakula mwaka huu ni mkubwa.

Brig. Jen. Mwangela amesema Mkoa una Hekta Milioni mbili ambapo zinazotumika katika Kilimo ni asilimia 30 tu huku eneo lingine likitumika katika makazi na Misitu lakini eneo kubwa linalobaki halijatumika bado.

Ameongeza kuwa Mkoa una eneo la hekta elfu 18 linalofaa kwa ajli ya kilimo cha Umwagiliaji na pia amewahakikishia vijana kuwa ardhi kwa ajili ya Kilimo Mkoa wa Songwe sio tatizo.

Brig. Jen. Mwangela amesema vijana wabadilike kifikra na kuanza kuthamini kilimo kwakuwa ili kupambana na umasikini vitendo vinahitajika Zaidi kuliko maneno tu ya kulalamika.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe Eliniko Mkola amesema vijana wa Kitanzania waliopata mafunzo ya Kilimo Nchini Israel wasikae na elimu hiyo bali wawaelimishe vijana wenzao na mashamba yao yatumike kama madarasa ya kujifunzia Kilimo.

Mkurugenzi wa SUGEC Revocatus Kimario amesema taasisi yake inajihusisha na kuwasaidia vijana katika Sekta ya Kilimo na moja ya changamoto ni mtamzamo wa vijana juu ya kilimo.

Kimario amesema walimu pia wamechangia kutengeneza mtazamo hasi juu ya kilimo kwa kuwa wamekuwa wakitoa adhabu zinazohusiana na Kilimo pale ambapo mwanafunzi anafanya makossa.

“Vijana hawapendi kilimo kwakuwa wamezoe kulima kama adhabu wanapokuwa shuleni, unataka akimaliza masomo akafanye kitu ambacho amekijenga kuwa ni adhabu?, Kilimo ni ajira hivyo waalimu wanapaswa kuacha kukitumia kama adhabu kwa wanafunzi.”, amesema Kimario.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Songwe Hassan Lyamba ameipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuandaa Kongamano hilo kwakuwa litawafungua akili vijana juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Kilimo.

Lyamba ameongeza kwa kuwataka vijana kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo yale yote waliyo jifunza katika kongamano hilo ili wawe sehemu ya mabadiliko katika sekta ya Kilimo nchini.

Kauli Mbiu ya Kongamano la Vijana ambalo linatarajiwa kufanyika nchini Kote katika Kanda Saba ni; “Vijana, Kilimo ni Ajira”.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne February 25

Mangula Alia Na Amani Ya Tanzania

$
0
0
 Na John Mapepele
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula  amewataka watanzania kutochezea  amani  na  kuyumbishwa na wanasiasia  na badala yake  waione amani walio nayo kama mtaji mkubwa wa kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kizazi cha sasa na baadaye.

Mangula ameyasema haya leo katika ukumbi wa maktaba Manyoni wakati alipohitimisha ziara yake ya kikazi ya siku saba kwenye Mkoa wa Singida ambapo amesema Tanzania  ni miongoni mwa nchi chache duniani ambayo imebahatika kuwa amani katika kipindi chote kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Alisema hivyo ni wajibu  wa kila mwananchi mzalendo  kuilinda kwa kuwa  watu wengi hawapendi kuona Tanzania  ina amani na kupiga maendeleo ya haraka kama inavyofanya sasa.

“Ndugu zangu hata tukichukulia mfano mdogo tu, katika kipindi cha miaka 75 ambayo tulitawaliwa na Wajerumani na Waingereza kwenye Wilaya yote ya Manyoni  hatukuwa hata na Shule mmoja ya Sekondari lakini  leo tuna zaidi ya shule 30 katika kipindi kifupi, je hayo siyo maendeleo makubwa ?” alihoji Mangula

Alisisitiza kuwa mapinduzi  makubwa  ya kiuchumi yanayofanywa  na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli yanatokana na  msingi  imara uliojengwa ambao ni amani na kwamba wachafuzi wa kubwa  wa amani dunani kote ni wanasiasa  ambao wamekuwa wakisukumwa na tamaa ya madaraka ambapo yakitokea  wanaoumia ni  watoto, wazee na akina mama.

Akitolea mfano wa machafuko ya kisiasa ya Rwanda ya mwaka 1994 alisema akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakati huo,  alishuhudia wimbi kubwa la watoto na akina mama wakiteseka  na kufa njiani wakati wakijaribu kukimbia nchi yao  kunuisuru maisha yao.

“Nilishuhudia  mama akina mama  wakitanda kanga na kumsaidia mama mwenzao kujifungua mtoto pembeni mwa barabara na baada ya kujifungua tu wakaendelea na  safari, kwa kweli  huwa sipendi kukumbuka  hali ile maana  ni  hatari na ukatili usioelezeka” aliongeza Mangula

Akiwa katika mkutano huo amesisitiza suala la uadilifu na kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za chama   cha Mapinduzi ambapo amesema vitendo vyoyote vya rushwa na wagombea kuanza kujipitisha kabla ya kipindi rasmi cha kuchukua fomu za kugombea na kuanza mchakato wa uchaguzi hakikubaliki na kusisitiza kuwa chama kitachukua hatua kwa wote watakao bainika kufanya hivyo.

Aidha Kamati za Siasa katika maeneo husika zitakazoshindwa kuwachukulia hatua wanachama watakaofanya makosa zitaadhibiwa.

Akiwa katika ziara hiyo ametembelea  miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Mkoa wa Singida ambapo mradi wa mwisho alioutembelea ni mradi mkubwa wa shamba la pamoja la Korosho lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 12000 eneo la Masagati kwenye Wilaya ya Manyoni na kusifu juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuleta mapinduzi makubwa  ya kilimo kwa wananchi bila kujali itikadi ya vyama vyao.

Amesema alama ya Chama Cha Mapinduzi ni jembe na nyundo ambapo amesema jembe ni alama ya mkulima  na nyundo ni mfanyakazi hivyo CCM inaamini kuwa  wakulima  na wafanyakazi wanamchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi yao na kuwa   mapinduzi ya uchumi hapa Tanzania yameletwa na kilimo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Danieli Mtuka akimwelezea Mangula kwenye shamba  la Korosho la Masagati ameshukuru Serikali ya Mkoa wa Singida chini ya Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi kwa kushirikisha wananchi katika  kuwabadili  mawazo na mtazamo wa kutafuta maendeleo ya kweli  kwa kulima shamba la pamoja la korosho ambapo amesema wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Mhe. Mtuka amesema kutokana na utafiti uliofanyika  na watafiti wa kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mazao ya Kilimo Naliendele kwa kushirikiana na watafiti wa mazao ya Kilimo Kanda ya Kati uliofanyika  kuanzia mwaka  2002, matokeo ya utafiti huo yalionyesha  kuwa hali ya hewa na udongo vinafaa kwa kilimo cha korosho hivyo wakaanza kuwahamashisha wananchi kulima zao hilo

“ Kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa na Halmashauri tuliamua kuanzisha zao la korosho kimkakati ili kuchochea kwa kasi kubwa  ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja wilaya,mkoa  na taifa kwa ujumla’” aliongeza Mhe. Mtuka


Aidha,alipongeza  Serikali ya Mkoa kwa kubuni wazo la kuanzishwa kituo kwa kikubwa cha  hija duniani cha Bikira Maria  katika eneo la Sukamahela, sehemu ambayo ni katikati ya nchi ya Tanzania  kwa ajili ya watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuhiji.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Charles Fussi amesema kuwa kazi  zinazoendelea katika eneo hilo kwa sasa  ni  kuhamasisha wakulima  wajiunge na kilimo cha korosho, kuendelea kutoa huduma za ugani kwa wakulima ikiwa ni pamoja na  matumizi sahihi ya viuatilifu kwa kushirikiana na TARI na Bodi ya Korosho, kuendelea kazi ya kusafisha na kugawa mashamba kwa wakulima na kuzalisha miche  bora  korosho.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Jackson Mwagisa  amemhakikishia Mangula kuwa serikali itaendelea  kusimamia kikamilifu  na kuwa hamasisha wananchi kutoka sehemu mbali mbali nchini  kuja kuwekeza katika  kilimo  cha korosho kwenye eneo hilo kwa kuwa mradi huo na manufaa makubwa kwa wananchi wa wilaya  ya Manyoni na Taifa kwa ujumla.

Ametaja baadhi ya manufaa ya mradi huo kuwa ni pamoja na  udhibiti wa  visumbufu kama magonjwa na wadudu,udhibiti wa  ubora wa korosho kutokana na usimamizi wa karibu, upatikanaji wa uhakika wa soko katika eneo la mradi,kurahisisha upatikanaji wa pembejeo na huduma za ugani ili kuhudumia eneo kubwa kwa wakati mmoja na chanzo kikuu  cha malighafi za viwanda vya kusindika korosho.

Manufaa mengine ya mradi ni kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri kupitia ushuru na kodi za biashara mbalimbali zitokanazo na ongezeko la uchumi katika sekta mtambuka zinazoendana na zao hilo, hali ya maisha  kuboreka ikiwa ni  pamoja na ujenzi wa makazi bora na kuongezeka  uhakika  wa chakula  katika kaya.

CODE.

Tanzania Yashinda Tuzo Ya Utalii Nchini India

$
0
0
Tanzania imeshinda tuzo ya utalii kwa kuonekana ni eneo bora zaidi la utalii wa wanyamapori duniani nchini India kwa mwaka 2020 (The Best International Wildlife Destination).

Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka H. Luvanda amepokea Tuzo hiyo kutoka Jarida la kihindi la “Outlook Traveller Magazine” katika hafla maalum iliyofanyika katika Hoteli ya Roseate jijini New Delhi kwa niaba ya Tanzania. Hafla hiyo ilihudhuriwa na takriban washiriki 200. 

Tanzania imepata ushindi huo kutokana na kura zilizopigwa kwenye mtandao wa jarida hilo la “Outlook Traveller” lililoshirikisha wapiga kura 1,200,000 kwa njia ya mtandao.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushinda tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka nchini India, washiriki kupitia jarida hilo wameichagua Tanzania kama eneo bora zaidi la utalii wa wanyamapori duniani.

Aidha, Shelisheli na Indonesia kwa pamoja zilishinda tuzo kama maeneo bora zaidi duniani kwenye utalii wa fukwe.

The Outlook Traveller Award ni tuzo ya kifahari zaidi katika sekta ya utalii nchini India na hutolewa na Jarida la Utalii la “Outlook Traveller Magazine” ambalo ni jarida namba moja nchini India linalojishughulisha kutangaza utalii, ndani na nje ya India.

Wakati akipokea tuzo hiyo, pamoja na mambo mengine Balozi Luvanda aliushukuru uongozi wa Jarida hilo kwa kuandaa tuzo hizo muhimu ambazo zinasaidia kutanganza utalii wa nchi mbalimbali nchini India na akaeleza kuwa kupitia tuzo hiyo, watu wengi zaidi wataijua Tanzania na vivutio vingi vya utalii vilivyopo nchini na kuwavutia kutembelea Tanzania.

Mafanikio hayo yanatokana na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini India, Wizara za Utalii za Tanzania Bara na Zanzibar, na Taasisi zote zinazosimamia masuala ya utalii za ndani na nje ya nchi katika kutangaza vivutio vya utalii kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo India.

Kupitia juhudi hizi, idadi ya watalii wanaokuja Tanzania kutoka India imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, idadi hiyo iliongezeka kutoka watalii 39,115 mwaka 2016 hadi watalii 69,876 mwaka 2017. 

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Balozi zake ukiwemo Ubalozi wa Tanzania nchini India na wadau wengine itaendelea kuongeza juhudi za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania ili kuhakikisha idadi ya watalii kutoka India na nchi zingine duniani inaongezeka. Hii ni pamoja na kutumia Shirika la Ndege la Tanzania ambalo limeanza safari za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Mumbai kuanzia mwezi Julai 2019 kwa upande wa India.

Ratiba ya michezo ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa 5

Tanzania Yaweka Wazi Mikakati Kufanikisha Uzalishaji Na Usambazaji Wa Nishati Ukanda Wa SADC

$
0
0
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
SERIKALI ya Tanzania imeweka wazi mipango na mikakati yake ya ufanikishaji wa malengo ya makubaliano ya kukuza uzalishaji, kujenga miundombinu na usambazaji wa nishati katika Nchi 15 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yaliyofikiwa na Viongozi Wakuu wa Kitaifa na Mawaziri wa sekta ya Nishati katika Jumuiya hiyo Mwezi Agosti mwaka 2019.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wataalamu wa nishati kutoka Nchi za SADC unaoendelea Jijini Dar es Salaam leo Jumanne (Februari  25, 2020), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said alisema mkutano huo unalenga kuanisha vyanzo na miradi mbalimbali ya kimkakati itakayowezesha utoshelevu wa nishati katika nchi za SADC.

Mhandisi Zena alisema kupitia Mkutano wataalamu wa sekta ya nishati wa Tanzania wataweza kubainisha fursa zilizopo katika kuhakikisha utoshelevu wa sekta ya nishati nchini ikiwemo Ujenzi wa Mradi Bwawa la kuzalisha Umeme kwa Kutumia maporomoko ya maji ya Bonde la Mto Rufiji wa Julius Nyerere (JNHPP) unaotarajia kuzalisha unaotarajia kuzalisha Megawati 2115.

‘’Tumeshuhudia majanga mbalimbali yanayotokana na mabadiliko ya baia nchi, sasa wataalamu wetu wa masuala ya nishati, mafuta na gesi watakutana na kujadili kwa pamoja ili kupata njia bora zaidi za kuweza kuzalisha nishati ya umeme itakayoweza kuwasaidia wananchi wetu’’ alisema Mhandisi Zena.

Alisema mipango na mikakati ya kuimarisha sekta ya nishati katika ukanda wa SADC ni utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Viongozi wa Kitaifa na Mawaziri wa sekta ya nishati katika Jumuiya ya SADC na Tanzania imepanga kuutumia vyema mkutano huo ili kuhakikisha kuwa sekta ya nishati inakuwa ya kibiashara na hivyo kuweza kutengeneza fursa kwa Watanzania.

Kwa mujibu wa Mhandisi Zena alisema mkutano huo wa wataalamu unatarajia kuhitimishwa mwishoni mwa wiki hii, ambapo mwezi Mei mwaka huu kunatarajia kufanyika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa sekta ya nishati katika Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC, ili kuona namna bora zaidi ya utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kuleta tija na maendeleo endelevu kwa wananchi wa ukanda wa SADC.

Aliongeza kuwa mbali na miradi hiyo ya kimkakati, wataalamu hao hao pia watajadili fursa za nishati jadidifu na namna zinavyoweza kuongeza uwezo wa upatikanaji wa nishati ya umeme ili kuwawezesha wananchi wa ukanda wa SADC kuweza kuwa na nishati ya uhakika na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa yanayochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.

Kwa upande wake Kamishna wa Nishati na Gesi kutoka Wizara ya Nishati, Adam Zuberi alisema mkutano huo umeshirisha jumla ya nchi wanachama 12 wa Jumuiya hiyo, ambao wanaandaa maazimio mbalimbali yanayotarajiwa kujadiliwa katika Baraza la Mawaziri wa sekta ya Nishati wa Jumuiya hiyo mwezi Mei mwaka huu.

Aliongeza kuwa katika mkutano huo, wataalamu hao pia watapata fursa ya kushiriki semina zitakazohusisha uwasilishaji wa mada na makongamano mbalimbali ya wadau wa sekta ya nishati ndani ya ukanda wa SADC.

UNESCO Yatambua Kiswahili Kama Lugha Itakayosaidia Kukuza Utangamano Barani Afrika

$
0
0
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeitambua Lugha ya Kiswahili kama lugha itakayosaidia kukuza utangamano Barani Afrika wakati wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yenye kaulimbiu “Lugha Bila Mipaka” iliyofanyika jijini Paris, Ufaransa hivi karibuni.

Katika kuadhimisha siku hiyo, Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa kwa kushirikiana na UNESCO uliandaa mjadala kuhusu "Fursa na Changamoto za Kukitambua Kiswahili kama Lugha rasmi ya Bara la Afrika kwa ajili ya kukuza Utangamano".

Akizungumza wakati wa Mjadala huo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu katika UNESCO, Mhe. Samwel Shelukindo pamoja na mambo mengine, alieleza hatua iliyochukuliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kukifanya Kiswahili kuwa moja ya lugha zitakazotumika katika Jumuiya hiyo.

Aidha, Mhe. Balozi Shelukindo alizipongeza nchi za Afrika Kusini na Namibia kwa kuwa nchi za kwanza Kusini mwa Afrika zilizoamua kuanzisha ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili katika shule mbalimbali. Mjadala huo uliwashirikisha Wataalam mbalimbali akiwemo Prof. Aldin Mutembei kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,

Kufanyika kwa mjadala huo katika UNESCO ni moja ya juhudi zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa za kukifanya Kiswahili kuwa moja ya lugha zitakazotumika katika UNESCO.

Tanzania Yashiriki Kwa Mara Kwanza Katika Maonesho Ya Kimataifa Ya Bidhaa Za Kilimo Ya Paris 2020, Ufaransa

$
0
0
Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza katika Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Kilimo ya Paris 2020 yanayofanyika jijini Paris, Ufaransa kuanzia tarehe 22 Februari 2020 hadi tarehe 1 Machi 2020.

Maonesho hayo ambayo yalifunguliwa na Mhe. Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, yanatarajiwa kutembelewa na zaidi ya watu 600,000.

Wakati wa maonesho hayo, Tanzania itapata fursa ya kuonyesha bidhaa zake yakiwemo mazao ya kimkakati. Ujumbe wa Tanzania katika maonyesho hayo unaongozwa na Bw. Victor Rugemalila kutoka TANTRADE.

Ubalozi wa Tanzania ambao unaratibu maonesho hayo kupitia  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, unaishukuru Kampuni ya Tanzania Re-assurance (TAN-RE) ya Dar es Salaam, Tanzania, kwa kufadhili kwa kiasi kikubwa ushiriki wa Tanzania katika maonyesho. Aidha, Ubalozi unatambua mchango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Kampuni ya Kahawa  ya Inter State.

Changamoto Ya Umeme Na Utitiri Wa Kodi Vyalalamikiwa Mkoa Wa Mara

$
0
0


MWANDISHI WETU MUSOMA
Wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Mara wameelezea kero mbalimbali zinazochangia kukwamisha ukuaji wa uwekezaji mkoani humo ikiwemo tatizo la umeme na wengine kueleza changamoto za utitiri wa kodi.

Wameeleza changamoto hizo Februari 24, 2020 wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikiliza changamoto za wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa wa Mara uliohusisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri kutoka Sekta mbalimbali ikiwemo Viwanda na Biashara na masuala ya Fedha wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki   uliofanyika Wilaya Musoma Mjini katika Mkoa wa Mara.

Lengo la mkutano huo lilikuwa kusikiliza changamoto na kero wanazokabiliana nazo katika maeneo yao ya  biashara na uwekezaji na kuzitatua, ambapo wameeleza namna utitiri wa kodi na kukatikatika kwa umeme kunavyochangia uzorotaji kwa ukuaji wa uchumi na kuiomba Serikali kushughulikia tatizo hilo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Wafanyabiashara hao walieleza kuwa, kukosekana kwa umeme wa uhakika umekwamisha shughuli za uzalishaji ikiwemo zile za viwandani.

Kufuatia hali hiyo wameiomba Serikali kutatua kero hiyo huku wengine wakibainisha hasara wanazopata katika changamoto hiyo.

Akieleza changamoto za uwekezaji Dkt. John Changwa alieleza kuwa, TANESCO imechangia kukwamisha uzalishaji katika viwanda kutokana na  umeme kukatika mara kwa mara pamoja na kutofika kwa wakati katika viwanda vidogo kwa kuhusisha changamoto ya miundombinu hafifu ikiwemo barabara.

“Ni kweli kabisa TANESCO hamtutendei haki kwani mmekuwa mnatukwamisha kwa muda mrefu na mmeshindwa kufika kwa wakati hasa katika maeneo vinavyojengwa viwanda  huku  vikiwa vihitaji huduma za umeme hivyo ni vyema mkabadili utaratibu na kuona namna ya kutufikia kwa wakati,”Alieleza Dkt. Changwa

Akijibu baadhi ya kero hizo kwa kushirikiana na mawaziri wengine Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji Mhe. Angellah  Kairuki ametumia fursa hiyo kuzikumbusha Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini kusimamia kikamilifu utekelezaji wa maamuzi ya Serikali kwa kuhakikisha changamoto zilizoainishwa ikiwemo utitiri wa kodi, uwepo wa riba kubwa zinazotozwa na benki, ucheleweshwaji wa vibali vya ajira, ukosefu wa ajira kwa vijana, na uvuvi wa kutumia vyavu zisizokidhi mahitaji halisi na bei elekezi kuwa juu.
 
 ‘’Ni wakati sahihi kuendelea kuwahudumia wananchi kwa kuhakikisha tunatatua na kumaliza kero zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara ili kuendelea kuwa na maendeleo katika nchi yetu na niwahakikishie Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuwa na tija inayotakiwa,”alisema  Waziri Kairuki.

Sambamba na hilo alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara wa mkoa huo kuendelea kushirikiana na Serikali katika ulipaji wa kodi mbalimbali kwa utaratibu uliopo na kuhakikisha wanachangia katika ukuaji wa pato la taifa.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli inasisitiza ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya watanzania na taifa kwa ujumla hivyo lazima tuzingatie na kutimiza wajibu wetu ili kuepuka kuingia katika makosa yasiyo ya lazima na kupelekea uwekezaji wenu kuwa wa hasara”,alisisitiza Waziri Kairuki.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima alimhakikishia Waziri kuendelea kutatua kero na changamoto katika mkoa wake ili kuwahakikishia mazingira rafiki ya uwekezaji wao huku akiahidi kuendelea kusimamia sheria zote zinazowahusu ili kuwa na tija katika kuwekeza mkoani humo kwa kuzingatia fursa zilizopo.

“Mkutano huu umekuwa wa faida sana kwa kuzingatia umetoa fursa kubwa kwa kuwakusanya wafanyabiashara na wawekezaji 400 kwa pamoja na kuweza kuzieleza kero zao, tunaahidi kero ambazo hazijapatiwa majibu kwa siku ya leo zitatatuliwa haraka iwezekanavyo,”Alisisitiza Mhe. Malima.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>