↧
Darassa Kaachia DUDE La Nguvu Akimshirikisha Sho Madjozi – I Like It. ....Itazamahe Hapa
↧
PICHA: Rais Magufuli Na Mkewe Mama Janeth Magufuli Washiriki Ibada Ya Jumatano Ya Majivu Katika Kanisa La Mtakatifu Petro Jijini Dar Es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi wakati wa Ibada ya Jumatano ya Majivu jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020
Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi wakati wa Ibada ya Jumatano ya Majivu jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiondoka baada ya kuhudhuria Misa ya Jumatano ya Majivu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, akiongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli, akipakwa majivu na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi waliposhiriki Ibada ya Jumatano ya Majivu jijini Dar
es salaam leo Februari 26, 2020
PICHA NA IKULU
↧
↧
IGP Sirro Ataka Wazazi Waimarishe Malezi Kwa Watoto Ili Kuwa na Jamii Inayochukia Uhalifu
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro ametoa wito kwa jamii hasa wazazi nchini kuhakikisha wanaimarisha malezi ya watoto wao, jambo litalalosaidia kuwa na jamii itakayochukia uhalifu.
IGP Sirro ametoa wito huo mkoani Dodoma wakati akizungumza na baadhi ya Wakazi wa eneo la Mbande, baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha polisi katika eneo hilo.
Amewashauri wazazi wote nchini kuendelea kuwasomesha watoto wao na kutowaacha wajiingize kwenye vitendo vya uhalifu.
↧
Diamond Kadondosha Ngoma Mpya iitwayo JEJE......Itazame Hapa
↧
Algeria Yathibitisha Kuwa na Mgonjwa Wa Corona....Waliofariki Hadi Sasa Kwa Virusi Hivyo ni Watu 2,763
Algeria imethibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya Corona, ambapo mgonjwa ni raia wa Italia aliyewasili nchini humo Februari 17.
Tayari mgonjwa huyo amewekwa eneo maalumu la matibabu.
Algeria inakuwa nchi ya pili ya Afrika kupata muathirika wa virusi hivyo baaada ya Misri.
Watu waliofariki hadi sasa kwa virusi hivyo Ulimwenguni wamefikia 2,763 huku Watu 80,970 wakiathirika
Wagonjwa 29,745 wamepona maambukizi hayo nchini China na kuruhusiwa kutoka hospitalini

Watu 17 wafariki dunia na 150 wajeruhiwa katika Vurugu mjini New Delhi, India
Watu 17 wamefariki dunia na wengine wapatao 150 wamejeruhiwa hapo jana katika makabiliano kati ya waandamanaji wa makundi yanayokinzana mjini New Delhi huko India.
Makabiliano hayo ni mabaya zaidi kushuhudiwa tangu vurugu zilipozuka juu ya sheria mpya ya uraia mwanzoni mwa mwezi Desemba.
Vurugu hizo zilianza tangu mwishoni mwa juma lakini ziligeuka kuwa mbaya zaidi Jumatatu iliyopita.
Machafuko mapya yalianza tena jana Jumanne katika maeneo tofauti ya mji mkuu huo wa New Delhi.
Afisa wa idara ya kukabiliana na majanga ya moto ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba timu yake imekuwa ikipokea simu za dharura za kwenda kuzima moto katika maeneo tofauti.
Sheria hiyo mpya iliyozua ghasia inawapa fursa wahamiaji wasio Waislamu kutoka nchi tatu jirani kupata urai wa India.
Waislamu nchini India wanadai kuwa ni sheria ya kibaguzi.

Waasi wa Syria wanaoungwa mkono na Uturuki wadhibiti mji ulio karibu na Idlib
Waasi wa Syria wanaoungwa mkono na jeshi la Uturuki wamedhibiti mji wa Narab, katika mkoa wa Idlib, kwa mujibu wa vyanzo kutoka Uturuki na wawakilishi wa waasi.
Vikosi vya rais Bashar al-Assad, ambavyo vinaungwa mkono na jeshi la anga la Urusi, wanajaribu kuiteka ngome hii ya mwisho ya waasi nchini Syria baada ya miaka tisa ya vita.
Karibu raia milioni moja wameyahama makazi yao tangu kuanza tena kwa mashambulizi ya vikosi vya serikali vya Syria na mshirika wake Urusi Desemba mwaka jana, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.
Vikosi vya serikali vimeuteka mji wa Kafr Nabel na maeneo jirani, yanayopatikana karibu kilomita 30 Kusini Magharibi mwa Nairab, shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH), chanzo cha eneo hilo na vyombo vya habari vimeripoti.
Uturuki imetuma maelfu ya askari na vifaa katika mkoa huo kusaidia waasi wa Syria, na kuongeza mvutano na Urusi, mshirika mkuu wa Syria.
↧
Naibu Waziri wa Ardhi Angeline Mabula Atoa MAAGIZO Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuongeza kasi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa iliyopo Musoma mkoa wa Mara ili kukamilika kwa muda uliopangwa.
Hospitali hiyo ya Kwangwa ni ya ghorofa tano yenye shemu tatu (Wing A, B na C) na inarajiwa kuanza kutoa Huduma kwa baadhi ya sehemu kati kati ya mwezi ujao
Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana tarehe 25 Februari mjini Musoma mkoa wa Mara wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo unaofanywa na NHC akiwa katika ziara yake ya siku moja.
Alisema, pamoja na NHC kufanya vizuri katika ujenzi wa jengo la hospitali hiyo ukilinganisha na wakandarasi waliotangulia lakini inapaswa kuongeza kasi ili likamilike katika muda uliopangwa na kuanza kutoa huduma.
Kwa mujibu wa Mabula, Hospitali ya Kwangwa itakayojulikana kwa jina la Mwl Nyerere Memorial Hospital ina historia ndefu kwa kuwa pamoja na kuasisiwa na Rais wa Kwanza Mwalimu Julius Nyerere lakini utekelezaji wake unakamilishwa na serikali ya awamu ya tano.
‘’Ni vyema NHC mkaongeza bidii katika ujenzi wa hospitali hii ili ikamilike kwa haraka kwa kuwa hospitali hii ina historia ndefu na Rais John Pombe Magufuli ameamua ujenzi huu ukamilike kwa kutoa bilioni 15’’ alisema Mabula.
Katika kuhakikisha ujenzi wa hospitali hiyo unakamilika kwa wakati, Naibu Waziri Mabula alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa NHC Dkt Maulid Banyani kusimamia kwa karibu maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kupatiwa ratiba ya mpango wa ujenzi na maendeleo yake kila baada ya siku mbili kwa nia ya kufuatilia kwa karibu.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani alimuahakikishia Naibu Waziri Mabula kuwa, ujenzi wa hospitali hiyo sasa utakamilika kwa wakati baada ya changamoto kadhaa ikiwemo ya Mshauri Mwelekezi kupatiwa ufumbuzi.
Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima mbali na kuisifu NHC kwa kufanya mabadiliko makubwa ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa hospitali ya Kwangwa alioueleza kuwa ilikwamwa kwa mara kadhaa.
‘’Toka Shirika la Nyumba la Taifa lianze ujenzi wa hospitali hii mwezi Agosti mwaka jana kuna mabadiliko makubwa ya kasi ya ujenzi na tunataka mjenge kwa wakati na viwango na Machi mwaka huu Huduma ya Mama na Mtoto ianze kutolewa ‘’ alisema Malima.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, hospitali hiyo itatoa huduma kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya ziwa pamoja na nchi jirani sambamba na kutumika kama sehemu ya utalii kutokana na mazingira ya hospitali.
Historia ya Ujenzi wa Hospitali ya Kwangwa iliyopo Musoma mkoa wa Mara inaanzia mwaka 1977 pale Rais wa kwanza wa Mwl Nyerere alipotoa wazo la kujengwa kwake lakini ujenzi huo umekuwa ukikwama kwa nyakati tofauti hadi Rais John Pombe Magufuli alipotoa Shilingi Bilioni 15 kwa lengo la kukamilishwa mradi huo ambapo sasa unatarajiwa kukamilika mwaka huu.
↧
Naibu Waziri Josephat Kandege Afurahishwa Na Miradi Ya TARURA – Ilemela Jijini Mwanza....Wananchi Nao Waimwagia Sifa Serikali Kwa Kuwainua Kiuchumi
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege ameelezea kuridhishwa kwake na miradi ya barabara iliyotekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tarura katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
Aliyasema hayo wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Mwanza ambapo ameeleza kuwa mafanikio yanayopatikana katika Manispaa hiyo hasa katika miradi ya barabara yanatokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya wataalam wa TARURA na watumishi wengine wa Manispaa kwa kufanya kazi pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi.
‘‘ Wote tumeshuhudia barabara hizi zilivyo kwenye kiwango, mafanikio haya yanatokana na Umoja uliopo kwa watumishi wote wa Manispaa ya Ilemela pamoja na watumishi wa TARURA kwani wanafanya kazi kwa pamoja ili kuwaletea wananchi wetu maendeleo, kiujumla wanafanya vizuri’’Kandege.
Aidha amesisitiza kuwa miundombinu ya barabara inapokamilika ilindwe kwa nguvu zote na amewaagiza viongozi husika huhakikisha barabara hizo zinafanyiwa usafi mara kwa mara na kulinda miundombinu ya barabara hizo.
Naye Meneja wa TARURA Manispaa ya Ilemela Mhandisi Clement Kihinga amesema kuwa barabara hizo zilizotekelezwa chini ya mradi wa Tanzania Strategic Cities Project (TSP) zimekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuinua uchumi wa wananchi na kuboresha kiwango cha maisha ya wananchi.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanailinda miundmbinu ya barabara ilizidumu na ziendelee kuboresha maisha yao na kurahisisha suala la usafiri na usafirishaji katika Manispaa ya Ilemela.
‘‘Serikali inatumia gharama kubwa sana kujenga barabara hizi hivyo nitoe wito kwa wananchi kuhakikisha kila mmoja wetu anashiriki kulinda miundombinu hii ya barabara ’’ amesema Mtaalam huyo.
Mmoja wa wananchi wa Kiseke A Ilemela Issa Shabani alisema awali usafiri ulikuwa changamoto sana Katika barabar yao kwani miundombinu ilikuwa mibovu sana ila baada ya baraba ya kiseke Busweru kukamilika maisha yamepanda kiuchumi
“Sasa nafanya biashara yangu ya matunda hapa Busweru, nayabeba salama na hayaharibiki kwani barabara ni nzuri na hata kipato changu kimeongezeka hivyo naishukuru sana Serikali kwa kujenga barabara hii”Alisema Shabani
Ziara ya Mhe, Kandege inaendelea Mkoani Mwanza ambapo miradi mbalibali ya maendeleo zikiwemo barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA inatarajiwa kukaguliwa.
↧
↧
Bill Gates Ajitosa kupambana na nzige waliovamia Afrika Mashariki
Taasisi ya Bill & Melinda Gates imechangia dola za kimarekani milioni 10 (Tsh 23.1 bilioni) kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na nzige wavamizi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mchango huo utakabidhiwa kwa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) la Umoja wa Mataifa (UN) ambalo limekuwa likiwasihi watu na taasisi mbalimbali kuchangia fedha kukabiliana na nzige wanaohofiwa kusababisha njaa kutokana na kuvamia mazao.
Katika salamu zake za shukrani, Mkurugenzi Mtendaji wa FAO, QU Dongyu amesema hadi sasa UN imekusanya shilingi bilioni 76 za kitanzania, huku lengo likiwa ni kukusanya bilioni 318.
Nzige hao wamevamia nchi sita za Afrika Mashariki na wana uwezo wa kula chakula sawa na watakachokula watu 35,000 kwa siku moja wakiwa kwenye eneo la kilomita 1 ya mraba, FAO imeeleza.
Nzige hao wanazaliana kwa kasi kubwa sana katika mazingira rafiki ambapo ndani ya kipindi cha miezi sita wanauwezo wa kuongezeka kwa zaidi ya mara 500.
↧
TAKUKURU Yaagizwa Kuchunguza 'Waliotafuna' Fedha za Ujenzi Wa Choo Kahama
Serikali mkoani Shinyanga imetoa siku tatu kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilaya ya kahama kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha za ujenzi wa choo kipya cha shule ya msingi Bukondamoyo baada ya kubaini kutumika vibaya na kusababisha kutokamilika kwa wakati.
Agizo hilo limetolewa febuari 26 mwaka huu na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika shule hiyo iliyopo katika halmashauri ya mji Kahama ili kuona maendeleo ya ujenzi wa choo.
“Nilipata taarifa za upotoshaji katika mitandao ya kijamii zilizowekwa na watu wasiokuwa na nia nzuri na maendeleo ya shule hii kuwa shule hii haina choo, nimefika ili nijiridhishe nimebaini kamati ya shule hii imetumia fedha za wananchi vibaya katika ujenzi wa choo kipya”alisema Telack.
Telack aliwataka TAKUKURU kuhakisheni wananafanya uchunguzi wa kina ili kubaini ninani alihusika katika matumizi ya fedha za ujenzi wa choo hicho na kuwataka watu wanaosambaza taarifa kuwa shule hiyo haina choo kuacha mara moja kwani serikali tayari imeshachukua hatua za haraka kukabiliana na suala hilo baada ya choo cha awali kubomoka.
“Tayari mkurugenzi wa mji kahama ameshachukua hatua za haraka kwa kuleta vyoo vya dharura (mobile toilet) katika shule hiyo pamoja na kutoa fedha zaidi ya milioni 100 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo hivyo ili wanafunzi wawezekupata huduma nzuri”alisema Telack.
Awali akitoa taarifa za ujenzi wa choo hicho diwani wa viti maalum wa kata ya bukondamoyo Scholastika Danford alisema kuwa wananchi katika mtaa huo wamegoma kuchangia ujenzi wa choo hicho kutokana na kamati ya shule hiyo kutokuwa wawazi katika ujenzi kwa kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi.
“Sio kweli wananchi hawataki kuchangia maendeleo tatizo hapa hakuna uwazi shimo pekee la choo hiki linadaiwa kutumia zaidi ya shilingi milioni mbili jambo ambalo linawatia mashaka kuendelea kuchangia ujenzi huu”alisema Danford.
Aliongeza kuwa kamati ya shule hiyo imeshindwa kusimamia ujenzi wa choo hicho jambo ambalo limeilazimu halmashauri ya Mji kahama kuingilia kati kwa kutoa fedha kwaajili ya kujenga vyoo hivyo ili kuwawezesha wanafunzi kupata huduma hiyo baada ya vyoo vya awali kubomoka.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Modesta Kalisius alisema kuwa shule hiyo inawanafunzi 2467 na madarasa 11,matundu sita na uhitaji wa vyoo ni matundu 111.
“Wasichana wanahitaji matundu 61 na wavulana matundu 50 naiomba halmashauri ya ikamilishe ujenzi wa choo hiki kwani kilichopo majengo yake ni chakavu na yamejaa”alisema Modesta
Mwisho.
↧
Naibu Waziri Wa Ardhi Angeline Mabula Ataka Halmashauri Kutenga Maeneo Ya Uwekezaji...."Tengeni Maeneo Mapema Kuepusha Usumbufu Baadaye"
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kuanza kupanga maeneo ya uwekezaji katika sehemu ambazo miji inakuwa kwa kasi.
Dkt Mabula alisema hayo jana katika mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali na sekta binafsi kuhusiana na changamoto za uwekezaji katika mkoa wa Simiyu.
Alisema, kuna maeneo mengi nchini ambayo miji inaendelea kwa kasi hivyo halmashauri kupitia Wakurugenzi wake zinapaswa kuhakikisha zinatenga maeneo ya uwekezaji kwa lengo la kumuwezesha Mwekezaji atakapopatikana asipate tabu.
‘’Ni vizuri katika kipindi hiki ambacho baadhi ya miji inakuwa kwa kasi halmashauri zikatenga maeneo ya uwekezaji na kuyahaulisha kwa lengo la kuwarahisishia wawekezaji watakapokuja kuwekeza katika halmashauri husika’’ alisema Mabula
Aidha, Naibu Waziri Mabula amezitaka pia halmashauri kuhakikisha zinapanga miji maeneo yaliyopo pembezoni kwa kuanishwa matumizi yake kama vile kilimo, ufugaji na maeneo ya kuchezea kwa kutumia watendaji wa ngazi za chini badala ya kusubiri wataalamu wa mipango miji.
Alisema, upangaji miji mapema kwa kutumia watendaji wa ngazi za chini utasaidia wataalamu wa mipango mijini watakapokuja baadaye kutopata shida katika kupanga maeneo hayo hasa katika ile miji inayokuwa kwa kasi kwa kuwa miji hiyo itakauwa imepangwa na kuainisha matumizi mbalimbali.
‘’Hawa watendaji wa chini wakipewa elimu wataweza kuipanga miji yao kama ilivyokuwa wakati wa vijiji vya ujamaa maana sasa hivi mtu anaweza kujenga kiwanda katikati ya makazi ya watu’’ alisema Mabula.
Katika mkutano huo Manaibu Mawaziri kutoka sekta mbalimbali walitolea ufafanuazi baadhi ya changamoto zilizowasilishwa kwao kwa lengo la kurahisisha ufanyaji biashara itakaokuwa na tija.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Ashatu Kijaji alitoa ufafanuazi wa riba kubwa kwa taasisi na fredha na kubainisha kuwa serikali ya awamu ya tano imesikia kilio hicho na imekuwa ikisisitiza taasisi hizo kupunguza riba kufikia asilimia kumi na moja.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Musa Sima alisema lengo la serikali si kufungia biashara bali ni kutafiuta njia itakayowawezesha wawekezaji kufanya biashara katika mazingira mazuri na kubainisha kuwa mtendaji wa ofisi yake atakayekwamisha jitihada hizo basi taarifa itolewe ili hatua zichukuliwe.
Naye Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa alisema, wizara yake inafanya jitihada kubwa kuunganisha mikoa katika masuala ya miundombinu sambamba na kushughulikia maeneo korofi ili wawekezaji wafanye kazi zao kwa urahisi.
↧
Aliyewahi kuwa Katibu Uhamasishaji BAVICHA Ajivua Uanachama wa CHADEMA.......“Chadema imekuwa kampuni ya mtu binafsi na sio chama cha Siasa.”
Aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi/ Uhamasishaji wa Baraza la Vijana la Chama Cha demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Edward Simbeye Leo February 26, 2020 ametangaza kujivua uanachama wa CHADEMA, kwa kile alichokisema kutokuunga mkono baadhi ya mambo yanayoendelea ndani ya chama hicho cha Chadema na kwamba kwa sasa anatafakari chama gani cha kujiunga.
Sembeye amesema moja ya vitu vinavyokiumiza chama hicho, ni chama kuendeshwa kwa amri na matakwa ya Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho na si Katiba ya Chadema.
"Mambo ya Chadema yanatakiwa kuamuliwa kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na miongozo ya chama, leo yanaamuliwa kwa kauli na amri za Mbowe, Mwenyekiti ameamua kugeuza chama kuwa mali yake binafsi, lakini tukitoka nje tunawaaminisha umma kuwa chama hichi ni mali ya Watanzania.
Amesema, kutokana na kutokuwa na umoja na msimamo, matokeo yake wamepoteza hata majiji waliyokuwa wakiyaongoza.

Tanzania Yaihakikishia Jumuiya Ya Kimataifa Uchaguzi Huru Na Wa Haki
Tanzania imesema hatua zote ambazo zimechukuliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya mabadiliko katika sheria za vyama vya siasa,sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali na ile ya vyombo vya habari ina lengo la kuimarisha uwajibikaji na uwazi pamoja na kuhakiskisha misingi na tunu za Taifa zinaheshimiwa na kuendelezwa.
Akihutubia katika Kikao cha 43 cha Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linaloendelea Geneva nchini Uswisi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Prof. Palamagamba John Kabudi Mashariki ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania inaheshimu na itaendelea kuheshimu haki zote binadamu zikiwemo za kisiasa na kwamba sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina lengo jema la kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa Taifa lenye amani,umoja na utulivu.
Pia Prof. Kabudi ameifahamisha jumuiya ya Kimataifa kuwa mwaka huu Tanzania itafanya uchaguzi wake mkuu wa sita tangu kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa na kuihakikishia jumuiya hiyo kuwa uchaguzi huo utakuwa wa uwazi,huru na wa haki na kwamba Tanzania itaalika waangalizi mbalimbali wa uchaguzi watakaotaka kushuhudia namna Watanzania wanavyotekeleza moja ya haki zao za msingi katika suala la kidemokrasia kwa kuchagua viongozi wao.
Amesema Tanzania inaheshimu na itaendelea kutekeleza kwa vitendo haki zote za binadamu bila ubaguzi na kwamba madai yanayoishutumu Tanzania kukiuka haki za binadamu ni propaganda na haswa zinatokana na hatua kali zinazochukuliwa dhidi ya rushwa,ubadhirifu wa mali za umma,madawa ya kulevya,uzembe katika ofisi za umma pamoja na hatua zinazochukuliwa kulinda rasilimali na maliasili ya Tanzania kwa manufaa ya Watanzania.
Kuhusu masuala ya sheria mpya za huduma vyombo vya habari,na haki ya kupata taarifa Prof. Kabudi ameiambia jumuiya ya kimataifa kuwa sheria hizo mpya zilizotungwa na Bunge la jamhuri ya Muungano ina lengo la kuimarisha,kulinda na kuweka mazingira bora zaidi kwa waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa usalama na kwa kuzingatia taaluma sambamba na kuwawezesha kupata haki zao ikiwa ni pamoja na mishahara bora na mikataba ya kazi.
Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland mazungumzo yaliyolenga masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na mradi ambao Jumuiya ya Madola umeufanya kuhusu Tanzania.
Mradi huo umelenga kuangalia takwimu mbalimbali zinazohusu biashara kwa kuangalia nchi ambazo Tanzania inaagiza ama kuuza bidhaa zake kwa wingi katika nchi za Jumuiya ya Madola mradi ambao umeelezwa kuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania ambapo kwa sasa nchi za India na Afrika kusini ndizo kinara.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi Patricia Scotland amesema Tanzania ni mdau muhimu katika jumuiya hiyo na kwamba amefurahi kumkabidhi Prof. Kabudi nakala ya utafiti huo kwa niaba ya Tanzania jambo litakaloifanya Tanzania kuendelea kuangalia maeneo ya kujiimarisha katika ufanyaji wa biashara na nchi za Jumuiya ya Madola.
Mbali na masuala hayo ya mradi huo wa takwimu wa biashara kuhusu Tanzania uliofanywa bure na Jumuiya hiyo ya Madola pia wawili hao wamezungumzia masuala mengine ikiwa ni pamoja na namna Jumuiya hiyo na Tanzania zitakavyofanya kuongeza usawa wa jinsia,masuala ya haki za binadamu pamoja na uimarishaji wa mfumo wa mahakama nchini Tanzania.
↧
Tanzania Yakabidhiwa Takwimu Za Ufanyaji Biashara Kati Yake Na Jumuiya Ya Madola.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland mazungumzo yaliyolenga masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na mradi ambao Jumuiya ya Madola umeufanya kuhusu Tanzania.
Mradi huo umelenga kuangalia takwimu mbalimbali zinazohusu biashara kwa kuangalia nchi ambazo Tanzania inaagiza ama kuuza bidhaa zake kwa wingi katika nchi za Jumuiya ya Madola mradi ambao umeelezwa kuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania ambapo kwa sasa nchi za India na Afrika kusini ndizo kinara.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi Patricia Scotland amesema Tanzania ni mdau muhimu katika jumuiya hiyo na kwamba amefurahi kumkabidhi Prof. Kabudi nakala ya utafiti huo kwa niaba ya Tanzania jambo litakaloifanya Tanzania kuendelea kuangalia maeneo ya kujiimarisha katika ufanyaji wa biashara na nchi za Jumuiya ya Madola.
Mbali na masuala hayo ya mradi huo wa takwimu wa biashara kuhusu Tanzania uliofanywa bure na Jumuiya hiyo ya Madola pia wawili hao wamezungumzia masuala mengine ikiwa ni pamoja na namna Jumuiya hiyo na Tanzania zitakavyofanya kuongeza usawa wa jinsia,masuala ya haki za binadamu pamoja na uimarishaji wa mfumo wa mahakama nchini Tanzania.
↧
Wachina waliotaka kumpa Rushwa Kamishna Mkuu wa TRA Wahukumiwa
Raia wawili wa China, Zheng Rongman(50) na Ou Ya(47), wamehukumiwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu, kulipa faini ya Sh.Mil 1 kwa kila mmoja baada ya kukiri makosa ya kutoa rushwa.
Pia mahakama hiyo imetaifisha fedha kiasi cha Sh.Mil 11.5 walizotaka kutoa kama rushwa kuwa Mali ya Serikali.
Rongman ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ronglan International Industry and Trade Co. Ltd na Ya, wamehukumiwa kulipa faini na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakamani, Huruma Shaidi.
Katika hukumu hiyo, Hakimu Shaidi, alisema washtakiwa wametiwa hatiani kama walivyoshtakiwa.
Mahakama hii inawahuku kila mmoja kulipa faini ya Sh 1milioni na kiasi cha Dola za Kimarekani 5,000 ambacho ni sawa na Sh.Mil 11.5 ambazo zimetaifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Hakimu Shaidi alisema wawekezaji wote wanatakiwa wafuata sheria na taratibu zilizopo nchini, hivyo kosa walilofanya washtakiwa hao halikubaliki.
Awali, wakili anayewatetea washtakiwa hao, Steven Bwana akisaidiana na Peter Lyimo na Denis Mdoe, aliomba Mahakama iwapunguzie adhabu.
Bwana alidai kuwa washtakiwa hao ni kosa lao la kwanza na kupitia Kampuni yao, wameweza kutoa ajira kwa watanzania 100 na wana familia inayowategemea.
Akisoma maelezo ya washtakiwa, Wakili kutoka Takukuru, Ipyana Mwakatobe alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
Alidia Februari 24, 2020, washtakiwa hao walifika Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) yaliyopo Wilaya ya Ilala jijini hapa kwa ajili ya kuona na kuonana na Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Edwin Mhende.
Mwakatobe alidai siku hiyo ya tukio, saa 10:00 jioni, washtakiwa hao walionana na Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Mhende Ofisi kwake akiwa na Msaidizi wake, ambapo walimueleza kuwa wana tatizo na kodi na kwamba waliwasilisha nyaraka kadhaa wakidia kuwa wamekadiriwa kiwango kikubwa cha kodi, hivyo walimuomba Kamishna huyo atatue mgogoro huo.
Washtakiwa hao baada ya kumueleza hayo Dk Mhende, walitoa kitita cha fedha ambazo ni dola za kimarekani 5,000 na kumkabidhi Kamishna huyo, kama kishawishi ili aweze kuwasaidia katika suala lao la kodi, ambapo Kampuni yao ilipaswa kulipa kodi ya Sh 1.3bilioni.
Mwakatobe alidia kuwa Dk Mhende, alimuelekeza Msaidizi wake kuzihesabu fedha hizo alizopewa na washtakiwa hao na kubaini kuwa zilikuwa ni dola.za kimarekani 5,000 , ambazo ni noti 50 za dola mia moja kila mmoja.
↧
Jenerali Mabeyo Azindua Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo amezindua Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo amezindua Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Akizungumza leo Februari 26, 2020 wakati akizundua makao makuu hayo Jenerali Mabeyo amesema kuwa, JKT imekuwa yakupigiwa mfano kwa utendaji unaotokana na utekelezaji mzuri wa miradi yote waliyokabidhiwa.
“Nawapongeza JKT kwa kutekeleza kikamilifu miradi ya ujenzi wa ukuta wa Mirerani, Ujenzi wa ukuta wa Ikulu ya Chamwino, Ujenzi wa ukuta wa uwanja wa ndege Ngerengere,Ukamilishaji wa nyumba za Jeshi la Magereza Ukonga Jijini Dar es Salaam na miradi yote mliyokabidhiwa mlitekeleza kwa wakati, ubora na viwango hali iliyowajengea heshima “, Alisisitiza Jenerali Mabeyo
Akifafanua Jenerali Mabeyo amesema kuwa ni wakati muafaka kwa JKT kujipanga kwa kujiimarisha kwa kununua mitambo na vifaa zaidi ili kujenga uwezo wa kuendelea kutekeleza miradi mikubwa pasipo kutegemea vifaa na nyenzo za kukodi au kuazima.
Aliongeza kuwa ili kuendelea kujenga heshima ya JKT kwa Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Pombe Magufuli ni vyema utekelezaji wa miradi yote ukaendelea kuwa katika ubora unaotakiwa, uzingatiaji wa Sheria ya manunuzi na taratibu zote zilizowekwa na Serikali.
Aidha, Jenerali Mabeyo amewaasa Maafisa na Watumishi wa Umma watakaotumia majengo ya makao makuu hayo kuyatunza ili yaweze kudumu kwa kuwa ujenzi wake umetumia rasilimali nyingi.
Katika hatua nyingine Jenerali Mabeyo amesema kuwa JKT inapaswa kujipanga kwa kuwa itahusika katika kutekeleza mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Ulizi wa Taifa katika Wilaya hiyo.
Uzinduzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT umefanyika Bwigiri Wilayani Chamwino mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Wakuu wa Jeshi hilo wastaafu, Maafisa wa ngazi mbalimbali,ss Watumishi wa Umma, Wananchi na viongozi wa Wilaya hiyo.
↧
↧
Kiwanda Cha Vifaa Tiba Simiyu Kuipunguzia MSD Uagizaji Wa Vifaa Tiba Nje Ya Nchi
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Kukamilika kwa kiwanda cha vifaa tiba vitokanavyo na zao la pamba kinachotarajiwa kujengwa Bariadi mkoani Simiyu kutaipunguzia Bohari ya dawa (MSD) uagizaji wa bidhaa hizo toka nje ya nchi kwa asilimia 38.3.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Mhe. Angella Kairuki kwenye mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliofanyika Februari 25, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali za biashara na uwekezaji na ufumbuzi wake.
“MSD imekuwa ikitumia zaidi ya shilingi bilioni 147 kununua dawa na vifaa tiba zaidi ya 19 kutoka nje ya nchi, tunaamini kwa kuanzisha kiwanda cha vifaa tiba vitokanavyo na pamba na bidhaa zingine 19 zikiwemo nguo za madaktari na wauguzi tunaamini tutaiondolea MSD uagizaji wa bidha hizo kwa asilimia 38.3,”alisema Mhe. Kairuki.
Amesema kiwanda hicho kitasaidia kufikia azma ya Serikali ya kuongezea thamani zao la pamba badala ya kuisafirisha, ambapo kwa sasa zaidi ya asilimia 70 ya pamba inasafirishwa nje ya nchi.
Aidha, Mhe Kairuki ametoa wito kwa wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu kutumia fursa za uwekezaji zilizopo katika viwanda vya ngozi, nyama,vyakula vya mifugo, viwanda vya mafuta ya kula; huku akiwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa biashara na uwekezaji, kupunguza kero ya utitiri wa kodi na tozo mbalimbali, kupunguza mamlaka za udhibiti wa kibiashara na kuondoa muingiliano wa mamlaka hizo.
Katika hatua nyingine Mhe. Kairuki ameupongeza uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa Simiyu kuwa mkoa wa kwanza kuzindua mwongozo wa uwekezaji nchini mwaka 2017 pamoja na kutekeleza mkakati wa Wilaya Moja Bidhaa Moja(One District One Product -ODOP).
Kwa upande wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema zabuni ya kiwanda cha vifaa tiba vitokanavyo na pamba kinachotarajiwa kujengwa Mkoani Simiyu imeshatangazwa na jiwe la msingi linatarajiwa kuwekwa mwezi Mei, 2020.
Naye mkuu wa mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema Bodi ya Pamba itoe viuadudu kwa wakulima wa pamba kwa wakati ili kudhibiti madhara yanayoweza kusababishwa na magonjwa huku akisisitiza bei ya pamba kupangwa mapema kabla ya msimu.
Aidha, Mtaka ameomba Waziri anayeshughulikia Uwekezaji kuona namna ya kuwasaidia wafanyabiashara na wawekezaji katika changamoto ya kufungiwa biashara zao, ambapo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakifungiwa biashara na viongozi au watendaji kutoka katika Taasisi au Ofisi mbalimbali za Serikali.
Naye Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Simiyu, Bw. Zebedayo King ameomba mabaraza ya biashara yafanyike kwa wakati ili wafanyabiashara waendelee kupata fursa ya kukutana na viongozi wa Serikali na Taasisi za Fedha na kujadili namna ya kutatua changamoto mbalimbali katika biashara na uwekezaji ikiwemo masuala ya kodi, kulipwa madeni yao kwa wakati pamoja na mazingira ya uwekezaji na biashara kwa ujumla.
Awali akiwasilisha changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba Mwenyekiti wa chama cha Ushirika Mkoa wa Simiyu(SIMCU) Charles Madata amesema baadhi ya wakulima hawajalipwa fedha zao na dawa hazitolewi kwa wakati, hivyo akaomba wakulima wasaidiwe kutatua changamoto hizo ili waone faida ya kilimo cha zao hilo.
Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliwahusisha viongozi wa Serikali wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji, Mhe. Angella Kairuki, Manaibu Waziri kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Ardhi na Makazi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira, Wizara ya Madini, Wizara ya ujenzi, Viongozi wa Mkoa, Viongozi wa Jumuiya za Wafanyabiashara, wakulima na Wajasiriamali
MWISHO.

Wanajeshi wa Syria Wanaosaidiwa na Urusi wakamata maeneo zaidi kutoka ngome ya waasi Wanaoungwa Mkono na Uturuki
Mashambulizi makali ya angani ya vikosi vya serikali ya Syria yamewauwa karibu watu watatu leo kaskazini mashariki mwa Syria, ambako vijiji kadhaa, zikiwemo ngome kuu za waasi katika eneo la mwisho linalodhibitiwa na upinzani, vimekamatwa katika siku chache zilizopita.
Machafuko hayo yamekuja wakati ujumbe wa Urusi ukitarajiwa kuwasili leo nchini Uturuki kuanzisha tena mazungumzo yanayolenga kupunguza mvutano katika mkoa wa kaskazini magharibi wa Idlib.
Zaidi ya watu 900,000 wamekimbia makazi yao katika karibu miezi mitatu.
↧
Serikali Yaweka Pingamizi Kesi Ya Tundu Lissu Kupinga kuvuliwa Ubunge
Serikali imemuwekea pingamizi la awali mbunge wa zamani wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu katika maombi yake ya kibali cha kukata rufaa kupigania ubunge wake, ikiiomba Mahakama Kuu iyatupe maombi hayo bila kuyasikiliza.
Lissu amefungua maombi hayo jijini Dar es Salaam dhidi ya Spika wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) akiomba kibali cha kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu suala hilo.
Awali Serikali ilifanikiwa kuishawishi Mahakama Kuu kutupa shauri la awali la mbunge huyo lililofunguliwa na kaka yake, Alute Mughwai aliyekuwa akiomba kibali cha kufungua shauri kutaka amri ya kutengua tangazo la Spika kuwa ubunge wa Lissu umekoma kutokana na utoro na kutojaza fomu za madeni na madili.
Katika uamuzi wake wa Septemba 9, 2019 uliotolewa na Jaji Sirilius Matupa, mahakama ilitupa maombi hayo ikikubaliana na hoja za Serikali kuwa Lissu hakupaswa kufungua maombi ya namna hiyo, bali alipaswa kufungua shauri la kupinga kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi yake.
Lakini Lissu hakukubaliana na uamuzi wala maelekezo, ndipo akafungua maombi mengine akiomba kibali cha kukata rufaa kupinga uamuzi huo.
Maombi hayo yalipangwa kusikilizwa jana na Jaji Yose Mlyambina, lakini yalikwama baada ya Serikali kuibuka na pingamizi la awali, ikiiomba maombi hayo ya Lissu yatupiliwe mbali, kwa hoja mbili.
Katika hoja hizo, Serikali inadai maombi hayo hayastahili kwa kuwa yanakiuka sheria na kwamba kwa kuwa yako kinyume cha sheria, basi ni ya usumbufu yanayolenga kuharibu taratibu za kimahakama.
Kufuatia pingamizi hilo la awali, mahakama imesimamisha usikilizwaji wa maombi ya Lissu badala yake ikasikiliza kwanza pingamizi hilo la Serikali, huku ikipanga kulitolea uamuzi Aprili 21, mwaka huu.
Uamuzi huo ndio utakaotoa hatima ya maombi hayo ya Lissu, ama kutupiliwa mbali au kuendelea kusikilizwa.