Mtuhumiwa mmoja kati ya tisa waliotiwa mbaroni na
jeshi la polisi baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika Kanisa la
Mtakatifu Joseph Mfanyakazi amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka
21 ya mauaji na kujaribu kuua. Victor Ambrose
Calist (20) ambaye ni dereva wa bodaboda na mkazi wa eneo la Kwa
Mromboo jijini Arushai amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu mkazi,
Devotha Kamuzora.
↧