Ndugu waandishi wa habari,Tumewaiteni hapa mchana huu kwa
dharula, kutokana na kujitokeza kwa jambo moja muhimu sana katika
mustakabali wa chama chetu na taifa kwa ujumla. Jambo lenyewe ni hili:Kwa muda
wa siku mbili, kuanzia kesho– tarehe 9 Julai 2013 hadi 10 Julai –
kutakuwa na “KONGAMANO LA AMANI” lililoitishwa na Kituo cha Demokrasia
Tanzania – Tanzania Center For Democracy (TCD).
↧