Tatizo la kukatika kwa umeme katika Jiji la Dar es Salaam litakwisha baada ya Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA kutoa msaada wa zaidi ya Sh bilioni 66, kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa vituo vipya vya kupozea umeme jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Felchesmi Mramba alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi
↧