MJUMBE wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khamis
Mgeja, amewataka baadhi ya viongozi wa chama hicho kuheshimu haki za
wanachama na kuacha siasa za kibabe na kibaguzi kwa kuchunga kauli zao.
Pamoja na hilo, amewataka viongozi hao kutambua hakuna mtu mwenye
hatimiliki ndani ya chama hicho ila kila mwanachama ana haki sawa ya
kukipigania na kukijenga wakati wote.
↧