MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametoa kali
ya mwaka baada ya kunaswa akiingia ‘supermarket’ akiwa ametinga taulo.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika mji wa Maryland nchini
Marekani ambapo staa huyo amekwenda kwa ajili ya kufanya shoo kisha
kupigwa picha hiyo na rafiki yake ambaye aliiweka mtandaoni ikimuonesha
akiwa amefunga taulo kwenye matiti.
↧