Wanafunzi 48 wasichana wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari ya
vipaji maalum ya Muungano wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro
wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto na vifaa vyao
vyote.
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo ya wananchi Mh Zawadiel Maruchu
amesema, moto huo ulianza kwenye bweni hilo kuanzia saa moja usiku
wakati wanafunzi wakijiandaa kupata chakula
↧