WATU wawili wamekufa mkoani Singida katika matukio tofauti yaliyotokea hivi karibuni, likiwemo la mwanamke mmoja kupigwa na rungu na mumewe kutokana na kile kinachodhaniwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema kuwa tukio la kwanza lililotokea kijiji cha Songambele, kata ya Ndago wilayani Iramba Januari 11 mwaka huu majira ya saa 1.00
↧