Mahakama ya Rufani imetupilia mbali maombi ya marejeo kuhusu
uhalali wa uamuzi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam kuwafutia mashtaka ya
ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Joseph Ludovick
Rwezahura.
Hatua hiyo ya mahakama imefanya kiongozi huyo wa
Chadema na mwenzake kuibwaga Serikali kwa mara ya pili
↧