Mahakama ya kimataifa ya ICC imetupilia mbali kesi ya jinai inayomkabili
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Mwendesha mkuu wa mashitaka Fatou Bensouda ameondoa kesi dhidi ya
Kenyatta ambaye alidaiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa
ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007/2008.
Mahakama ilikuwa imempa Bensouda wiki moja kuamua ikiwa ataendelea na kesi dhidi ya Kenyatta au la.
↧