Mahakama
ya mwanzo Makete mjini wilayani Makete mkoani Njombe imemuhukumu katibu
wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya hiyo Bw Godfrey
Mahenge (63) kwenda jela miezi 9 kwa kosa la kutotii amri halali ya
jeshi la polisi Makete
Akitoa
hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo Makete mjini Mh. John
Mpitanjia amesema mtuhumiwa huyo alitumia lugha ya matusi kwa askari
polisi
↧